Mauaji na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake vimeongezeka nchini Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i96890-mauaji_na_vitendo_vya_ukatili_dhidi_ya_wanawake_vimeongezeka_nchini_tunisia
Wanawake wa Tunisia wanakabiliwa na hali mbaya ya ongezeko la ukatili na mauaji dhidi yao yanayofanywa na waume zao au na ndugu wa familia zao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 01, 2023 21:59 UTC
  • Mauaji na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake vimeongezeka nchini Tunisia

Wanawake wa Tunisia wanakabiliwa na hali mbaya ya ongezeko la ukatili na mauaji dhidi yao yanayofanywa na waume zao au na ndugu wa familia zao.

Mashirika ya haki za binadamu nchini Tunisia yametangaza kuwa, idadi ya wanawake waliouawa katika mikoa tofauti nchini humo tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2023 imefikia watu 9.  

Idadi ya vifo mtawalia vya wanawake huko Tunisia vinaongezeka katika kiwango cha kushtusha licha ya nchi hiyo kutambulika kama kinara wa kuheshimu haki za wanawake miongoni mwa nchi za Kiarabu.

Wanawake Tunisia wakabiliwa na ukatili mkubwa 

Watetezi wa haki za binadamu huko Tunisia wamelaani utekelezaji dhaifu wa mahakama wa sheria namba 58 ya mwaka 2007 na kushindwa kuchukua hatua viongozi wa vyombo vya usalama na mamlaka husika za nchi hiyo ili kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake. 

Ahlam al Hamami mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Tunisia anasema kuwa: Mauaji ya wanawake huko Tunisia yanatisha kufuatia kujiri visa 9 vya mauaji katika miezi mitatu iliyopita. Amesema kiwango hiki cha mauaji kinaonyesha kuwa kiujumla vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake nchini humo vimeongezeka.