-
UN yasikitishwa na kuendelea mashambulizi dhidi ya raia nchini Sudan
Mar 26, 2025 22:50Msemaji Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kuendelea mashambulizi dhidi ya raia nchini Sudan, ikiwa ni pamoja na shambulio baya la anga lililofanywa kwenye soko la Darfur Kaskazini, kumeutia wasiwasi mkubwa umoja huo.
-
Rais Ruto: Mwanasheria Mkuu aliyefutwa kazi alichelewesha tume ya wakfu wa Waislamu
Mar 26, 2025 09:21Rais William Ruto wa Kenya amemkosoa hadharini aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Justin Muturi, akitaja kipindi chake cha uongozi kuwa "kisichofaa" katika kushughulikia masuala muhimu ya kisheria, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Tume ya Wakfu wa Kiislamu. Kwa muda mrefu uanzishwaji wa mfuko huo umekuwa kilio cha Waislamu wa Kenya.
-
Tunisia yalaaniwa kwa kumkamata mwanachuo aliyepeperusha bendera ya Palestina
Mar 26, 2025 07:42Mwanafunzi mmoja wa Tunisia amekamatwa kwa kuingia uwanjani na kupeperusha bendera ya Palestina wakati wa mechi ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tunis.
-
Libya yawaachia huru wahamiaji 82 waliokuwa wametekwa na wahalifu
Mar 26, 2025 07:40Mamlaka za Libya zimetangaza habari ya kuwaachilia huru wahamiaji 82 waliokuwa wakishikiliwa mateka na kundi la wahalifu likidai kikomboleo.
-
Rwanda yapinga kauli ya rais wa Burundi kwamba inapanga kushambulia nchi yake
Mar 26, 2025 07:39Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda amesema kwamba kauli ya Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, kwamba Rwanda inapanga kushambulia nchi yake ni "ya kusikitisha."
-
Muungano wa Madaktari wa Sudan Kusini waitaka serikali kushughulikia mlipuko wa kipindupindu
Mar 26, 2025 04:18Muungano wa Madaktari wa Sudan Kusini (SSDU) umeitaka serikali kushughulikia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu unaoongezeka nchini humo. Ugonjwa wa kipindupindu tayari umeenea katika majimbo kadhaa ya Sudan Kusini na hivyo kuyaweka hatarini maisha ya maelfu ya watu.
-
Watu 54 wameuawa katika shambulio la anga linalodaiwa kufanywa na jeshi la Sudan
Mar 26, 2025 04:15Makundi ya misaada ya kibinadamu yameripoti kuwa watu wasiopungua 54 wameuawa katika shambulio la anga la jeshi katika soko moja mashariki mwa nchi hiyo.
-
Namibia: Hakuna raia wa Marekani atakayeingia nchini bila ya viza; utekelezaji kuanza Aprili Mosi
Mar 25, 2025 23:58Serikali ya Namibia imetangaza kuwa, raia wa Marekani wanaotaka kuitembelea nchi hiyo itawapasa wawe na viza kabla ya kuingia nchini humo.
-
UN yaonya tena: Sudan Kusini inakaribia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe
Mar 25, 2025 23:11Umoja wa Mataifa umeonya kuwa Sudan Kusini iko kwenye ukingo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huku ghasia kati ya pande zinazohasimiana zikiongezeka.
-
WFP yapunguza mgao wa chakula katika oparesheni zake nchini Burundi
Mar 25, 2025 23:10Ongezeko kubwa la wakimbizi wanaohitaji msaada limesababisha mashinikizo makubwa kwa oparesheni ya usambazaji misaada ya chakula ya Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP).