Jun 23, 2024 10:54 UTC
  • Droni ya Hud-hud ya Hizbullah yazusha kiwewe katika safu za Wazayuni + Picha

Ingawa vyombo vya habari vya serikali ya utawala wa Kizayuni vinapigana kufa na kupona kuchuja mno habari na kufifiliza athari za droni ya Hodhod ya Hizbullah ndani kabisa ya ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel lakini vinashindwa kuficha athari zake kubwa ikiwa ni pamoja na kiwewe kilichowakumba viongozi wa Israel.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim, operesheni ya kishujaa ya ndege isiyo na rubani ya Hizbullah ya Lebanon droni ambayo imepewa jina la Hodhod, imezusha kihoro na woga mkono katika nyoyo za viongozi na wakazi wa utawala wa Kizayuni wakati huu ambapo mgogoro kati ya Hizbullah na utawala wa Kizayuni umefikia kiwango cha juu kabisa tokea tangu mwezi Oktoba 2023.

Hizbullah ya Lebanon iliupa mshituko mkubwa utawala wa Kizayuni kwa kusambaza video ya moja ya droni zake iliyopenya ndani kabisa ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na kupiga picha katika masafa ya karibu mno; maeneo nyeti sana ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wachambuzi mbalimbali wanasema kuwa, miongoni mwa ujumbe uliomo kwenye video za droni hiyo ya Hodhod ya Hizbullah ni kwamba kama vita vikubwa vitatokea, basi harakati hiyo ya Kiislamu itashambulia moja kwa moja maeneo hayo muhimu mno ya Israel kadiri utawala wa Kizayuni utakavyoshambulia maeneo ya Lebanon, na haitochunga wala kujali chochote kama ambavyo Israel nayo haichungi wala kujali chochote. 

Sehemu ya kwanza ya video iliyotolewa na Hezbullah ya Lebanon ni mchanganyiko wa picha zilizorekodiwa na  maelezo kuhusu maeneo zilipopigwa picha hizo. Cha kushangaza zaidi ni kuwa droni hiyo ya Hizbullah ilifanikiwa kuingia maeneo nyeti mno ya utawala wa Kizayuni na kupiga picha kadiri ilivyopenda bila ya kugunduliwa na vyombo vya kijasusi na vya ulinzi vya Israel ambayo inajigamba kuwa eti ina jeshi na teknolojia za kisasa kabisa zisizoshindika.

Hapa chini tumeweka baadhi ya picha zilizopigwa na droni hiyo ya Hodhod ya Hizbullah na kuzusha kiwewe na uogofyaji mkubwa katika safu za wakazi na viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

 

Tags