Wananchi wa mataifa ya eneo wafurahia na kupongeza shambulio la kijeshi la Iran dhidi ya Israel + Picha
(last modified 2024-10-02T08:56:08+00:00 )
Oct 02, 2024 08:56 UTC
  • Wananchi wa mataifa ya eneo wafurahia na kupongeza shambulio la kijeshi la Iran dhidi ya Israel + Picha

Shambulio halali kisheria la makombora lililofanywa na Iran kwa kulenga maeneo ya kijeshi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, na ambalo limetekelezwa kutokana na kuuawa shahidi viongozi wa Muqawama, limeibua wimbi kubwa la furaha na matumaini kwa wananchi wa eneo la Magharibi mwa Asia.

Kwa mujibu wa IRNA, wananchi wa Lebanon walianza kufyatua fataki mitaani jana usiku mara tu walipopata habari kuhusu shambulio kubwa la makombora lililofanywa na Iran dhidi ya Israel.
 
Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza nao pia walisherehekea na kushangiria baada ya shambulio la makombora lililofanywa na vikosi vya ulinzi vya Iran dhidi ya utawala haramu wa Israel.
 
Makumi ya vijana wa Kipalestina walikusanyika pia karibu na Ukanda wa Natzarim huko Ghaza.
 
Katika mikanda ya video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, wanaonekana pia wananchi wa Iraq na Jordan wakicheza mabarabarani kushangiria na kupongeza jibu la Iran kwa utawala wa Kizayuni.
 
 Aidha, katika mkanda mwingine, vinaonekana vitafunio vitamu vikigawia katika programu ya mubashara ya chaneli moja ya televisheni ya Uturuki.
 
Inafaa kukumbusha kuwa baada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kujizuia kwa muda mrefu na kuonyesha stahamala na uvumilivu kwa ukiukwaji wa mamlaka yake ya kujitawala na vilevile kutokana na mauaji ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya Mashahidi Ismail Haniya, Sayyid Hassan Nasrullah, Meja Jenerali wa IRGC Sayyid Abbas Nilforoushan, mbali na mauaji ya halaiki ya wanawake na watoto wasio na hatia wa Palestina na Lebanon yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni, imeamua hatimaye kutumia haki iliyonayo kila nchi ya kujilinda kisheria kulingana na Hati ya Umoja wa Mataifa, kwa kutekeleza Operesheni ya Ahadi ya Kweli 2 kwa kushambulia ngome za utawala wa Kizayuni kwa mamia ya makombora ya balistiki.../

Baadhi ya picha za watu wa maeneo mbalimbali wakifurahi kipigo cha makombora kilichotolewa na Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ni kama ifuatavyo: 

 

Tags