-
Waislamu Kenya walalamikia marufuku ya Hijabu mashuleni + Sauti
Jan 24, 2019 13:16Waislamu nchini Kenya wamelalamikia uamuzi wa Mahakama ya Kilele ya nchi hiyo wa kubatilisha ruhusa ya wanafunzi wa kike kuvaa vazi la staha la Hijabu katika shule zote za nchi hiyo. Seifullah Murtadha na maelezo zaidi...
-
Tshisekedi aapishwa kuwa Rais mpya wa Congo DR + Sauti
Jan 24, 2019 12:27Kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi amepishwa leo kushika hatamu za uongozi wa nchi hiyo akimrithi Rais Joseph Kabila aliyemaliza muda wake. Hatua hiyo inahesabiwa kuwa ya kwanza katika nchi hiyo ya katikati mwa Afrika ya kukabidhiana madaraka kwa njia ya amani na ya kidemokrasia katika kipindi hote cha miaka 59 iliyopita.
-
Burundi: Kuna njama za kuvuruga uhusiano wetu na Tanzania + Sauti
Jan 21, 2019 14:51Mashirika ya Capes na Pisc ya nchini Burundi yamesema kuwa, kugunduliwa sare za jeshi la Tanzania katika kambi ya wakimbizi huko Burundi kunadhihirisha kuwepo njama za kutaka kuvuruga uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili. Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Bujumbura.
-
Washukiwa wanne wa ugaidi wajisalimisha nchini Kenya + Sauti
Jan 21, 2019 14:46Washukiwa wanne kati ya wanane waliokuwa wakisakwa na mamlaka za usalama nchini Kenya wamejisalimisha huku polisi wakizidisha msako kote nchini humo.
-
Uganda yaanzisha kampeni mpya ya kupambana na magonjwa hatari + SAUTI
Jan 19, 2019 14:48Serikali ya Uganda kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) imeanzisha upya kampeni ya kupambana na magonjwa kadhaa hatari ambayo yamezuka tena nchini humo. Kigozi Ismail na maelezo zaidi...
-
SAUTI, Ripoti ya matukio ya Kiislamu, Waislamu Tanzania walaani hatua ya kuvunjwa msikiti wa Chuo Kikuu Dodoma/ Waislamu Kenya walaani ugaidi
Jan 18, 2019 13:12Wanaharakati na watetezi wa haki za binaadamu nchini Tanzania wamelaani vikali kitendo cha Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dodoma, Petter Msoffe kusimamisha ujenzi wa msikiti chuoni hapo na kukitaja kitendo hicho kuwa kinakiuka haki ya binaadamu na uhuru wa kuabudu.
-
SAUTI, Burundi: Tutahudhuria mkutano wa EAC na tutautumia mkutano huo kuishitaki Rwanda
Jan 17, 2019 13:45Serikali ya Burundi imetangaza kwamba itahudhuria mkutano wa viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.
-
Jumuiya ya Waislamu Duniani: Burundi ni kiigizo chema+SAUTI
Jan 15, 2019 12:35Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Duniani yuko safarini nchini Burundi ambapo amehudhuria hii leo mkutano wa kusisitizia haja ya kutumiwa tofauti za kidini na kikabila kuimarisha utangamano.
-
Vijana wa NRM wazozana tena na Polisi nchini Uganda + Sauti
Jan 14, 2019 23:11Kwa mara nyingine tena, vijana wa chama tawala cha NRM nchini Uganda wamezozana na polisi wa nchi hiyo wakipinga ubeberu wa mkoloni Muingereza. Maelezo zaidi yamo kwenye ripoti ya mwandishi wetu wa Kampala, Kigozi Ismail...
-
Jeshi la Iran: Ndege iliyoanguka mapema leo nje ya Tehran ilikuwa ya mizigo + Video
Jan 14, 2019 04:53Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetoa taarifa kuhusu ajali ya ndege iliyotokea mapema leo asubuhi karibu ya mji wa Karaj nje ya Tehran na kusema kuwa, ndege hiyo aina ya Boing 707 ilikuwa ya mizigo na ilikuwa ikitokea Bishkek Kyrgyzstan.