Jenerali Ashtiani: US itakabiliwa na pigo zito iwapo vita vya Gaza havitamalizika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i104404-jenerali_ashtiani_us_itakabiliwa_na_pigo_zito_iwapo_vita_vya_gaza_havitamalizika
Waziri wa Ulinzi wa Iran ameonya kuwa, Marekani itakabiliwa na pigo kubwa na zito iwapo itashindwa kusimamisha mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 05, 2023 23:29 UTC
  • Jenerali Ashtiani: US itakabiliwa na pigo zito iwapo vita vya Gaza havitamalizika

Waziri wa Ulinzi wa Iran ameonya kuwa, Marekani itakabiliwa na pigo kubwa na zito iwapo itashindwa kusimamisha mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani alitoa indhari hiyo jana Jumapili na kuongeza kuwa, "Ushauri wetu kwa Wamarekani ni kukomesha vita hivi mara moja na kutekeleza makubaliano ya usitishaji vita, vinginevyo watapata pigo kubwa."

Brigedia Jenerali Ashtiani ameeleza bayana kuwa: Daima tumekuwa tukiwaasa Wamarekani wasiuunge mkono utawala wa Kizayuni.

Waziri wa Ulinzi wa Iran amebainisha kuwa, Marekani imefanya makosa kadhaa ya kistratajia hasa katika eneo la Asia Magharibi.

"Wamarekani na Waisraeli hivi sasa wapo kwenye kinamasi na wanatapatapa wakijaribu kujiondoa kwayo," ameongeza Jenerali Ashtiani.

Hujuma za kikatili za Israel huko Gaza

Brigedia Jenerali Ashtiani ameongeza kuwa, mahesabu yasiyo sahihi ya maadui ndiyo sababu ya kushindwa kwao mbele ya taifa la Iran tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini.

Waziri wa Ulinzi wa Iran ameeleza bayana kuwa, taifa la Iran limesimama imara na kishujaa mbele ya maadui ambao hadi hivi sasa wamefeli na wameshindwa kufikia malengo yao.