Iran na Ubelgiji zataka kuimarishwa ushirikiano
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i1372-iran_na_ubelgiji_zataka_kuimarishwa_ushirikiano
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema anataraji kuwa uhusiano wa kiuchumi kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Ubelgiji utaongezeka haraka katika kipindi hiki kipya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 16, 2016 11:38 UTC
  • Iran na Ubelgiji zataka kuimarishwa ushirikiano

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema anataraji kuwa uhusiano wa kiuchumi kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Ubelgiji utaongezeka haraka katika kipindi hiki kipya.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Muhammad Javad Zarif ambaye yuko ziarani huko Brussels kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa ngazi ya juu wa Ubelgiji amesema katika mazungumzo yake na Charles Yvon Michel, Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuwa nchi mbili zina suhula na nafasi nzuri ya kustawisha uhusiano katika nyanja mbalimbali ukiwemo uhusiano katika nyanja za nishati, sekta ya viwanda na teknolojia.

Pande mbili hizo pia zimeashiria kadhia ya wakimbizi, misimamo mikali na ugaidi na kueleza kuwa Iran na Ubelgiji zina fursa na vitisho vya aina moja vinazikabili na kwamba nchi mbili hizo zinapasa kuchukua hatua chanya ili kuimarisha uhusiano.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Waziri Mkuu wa Ubelgiji wamesema pia kuwa misimamo ya baadhi ya nchi inazidisha mgogoro wa Syria. Waziri Mkuu wa Ubelgiji ametaka pia kufanyike mashauriano na mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ukiwemo mgogoro wa Syria na kadhia ya wakimbizi na taathira zake kwa bara la Ulaya.