Mkutano wa usalama waanza mjini Tehran
Mkutano wa kwanza wa usalama umeanza kufanyika leo hapa mjini Tehran ukiwa na ajenda ya "usalama wa kieneo magharibi mwa Asia.
Imeelezwa kuwa, moja ya malengo ya mkutano huo uliofunguliwa kwa hotuba ya Dakta Ali Larijani, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuweko mazungumzo, hali ya kuaminiana na ushirikiano wa pamoja wa nchi za eneo la magharibi mwa Asia kwa shabaha ya kupatikana usalama na maendeleo ya wote.
Wanafikra amilifu katika masuala ya usalama wa eneo hili kutokana nchi mbalimbali wanashiriki katika mkutano huo lengo hasa likiwa ni kuwa na ufahamu kuhusiana na eneo hilo na hivyo kuweka mikakati ya kudumisha amani na usalama wa wote.
Mkutano huo wa kwanza wa usalama unafanyika hapa mjini Tehran kwa ubunifu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Imepangwa kuwa, wakati wa kufanyika mkutano huo kufanyike vikao sita vya kitaalamu kuhusiana na masuala ya usalama.
Lengo la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran la kubuni mkutano wa kiusalama wa Tehran ni kufanyika juhudi za kunufaika na kiigizo kilichofanikiwa cha ushirikiano wa makubaliano ya nyuklia katika kuleta nidhamu na kuweka mikakati mipya ya kiusalama katika eneo la magharibi mwa Asia.