Mar 17, 2016 13:39 UTC
  • Iran yalaani shambulio la kigaidi nchini Nigeria

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani shambulio la kigaidi lililofanywa katika msikiti mmoja huko Nigeria.

Katika radiamali kwa shambulio la kigaidi dhidi ya msikiti mmoja katika mji wa Maiduguri makao makuu ya jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria, Sadiq Hussein Jaberi Ansari, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametaka kuchukuliwa hatua za pande zote ili kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi.

Jaberi Ansari ametoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa shambulio hilo la kigaidi huko Nigeria na kueleza kuwa, kukaririwa jinai kama hiyo katika maeneo mbalimbali duniani, kunaonyesha kuwepo udharura wa kuchukuliwa hatua za lazima ili kukabiliana ipasavyo na kwa pande zote na ugaidi na suala la uchupaji mipaka.

Mlipuko uliotokea jana katika msikiti mmoja huko Maiduguri makao makuu ya jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria umeuwa watu 22 na kujeruhi wengine wengi; shambulio ambalo kundi la Boko Haram limetangaza kuwa limehusika.

Tags