MintPress News: Marekani imefadhili machafuko ya hivi karibuni nchini Iran
Mtandao wa habari wa Marekani wa MintPress News umefichua kwamba, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani imefadhili machafuko yaliyotokea hivi karibinu nchini Iran kwa kutoa zaidi ya dola milioni moja.
Mtandao wa MintPress News wenye makao yake makuu katika jimbo la Minnesota umefichua kwamba umepata waraka kutoka Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya nchi hiyo unaooneshawamba serikali ya Washington imechangia dola zaidi ya milioni moja kwa ajili ya machafuko ya hivi karibuni nchini Iran.
Ripoti iliyochapishwa na mtandao huo inasema kuwa: Marekani inatumia machafuko hayo kudhoofisha Utawala wa Kiislamu nchini iran kwa kufadhili makundi ya wapinzani wa Jamhuri ya Kiislamu na vyombo vya habari vinavyopiga vita Iran kwa kutenga makumi ya mamilioni ya dola kila mwaka. Vyombo hivyo vya habari vinatumiwa na Marekani kusambaza habari za uongo na zisizo za kweli dhidi ya Iran.
Nyaraka kadhaa rasmi za serikali ya Marekani zilizotolewa na Idara ya Huduma za Kongresi ya nchi hiyo pia zimeweka wazi mwelekeo wa serikali ya Donald Trump wa kuzusha machafuko na uharibifu nchini Iran.
Rais Donald Trump wa Marekani na maafisa kadhaa wa serikali yake walitangaza waziwazi uungaji mkono wao kwa machafuko na watu walioanzisha fujo za hivi karibuni hapa nchini.