Maandamano ya wananchi wa Iran baada ya Sala ya Ijumaa kupinga Marekani
Mamilioni ya wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo wanatazamiwa kushiriki katika maandamano makubwa baada ya Sala ya Ijumaa kulaani Marekani na sera zake za kiistikbari na ukiukaji wa ahadi.
Katika maandamano hayo yatakayofanyika katika miji yote mikubwa na midogo kote Iran wananchi wa Iran wanatazamiwa kulaani vikali utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani ambao umejiondoa katika mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji JCPOA. Katika Taarifa Idara ya Uhubiri wa Kiislamu imesema: "Hatua ya upande moja ya kiwendawazimu ya Donald Trump kujiondoa katika JCPOA ina lengo la kushadidisha vita vya kisaikolojia na mashinikizo ay kiuchumi dhidi ya watu wa Iran." Idara hiyo imetoa wito kwa wananchi wa Iran kujitokeza katika maandamano hayo dhidi ya Marekani na Utawlaa wa Kizayuni baada ya sala ya Ijumaa kote nchini.
Jumanne usiku Rais wa Marekani alitangaza uamuzi wa upande mmoja wa kuiondoa nchi yake katika mapatano ya nyuklia ya Iran ya JCPOA.
Hatua hiyo ya Marekani imepingwa na nchi zingine tanzo zilioafikia mapatano hayo ambazo ni China, Russia, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, ambazo zimetoa taarifa zikisisitiza kufungamana na mapatano hayo muhimu ya nyuklia.