Hatami: Kuwaunga mkono magaidi; njama ya maadui kwa ajili ya kuidhoofisha Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i47230-hatami_kuwaunga_mkono_magaidi_njama_ya_maadui_kwa_ajili_ya_kuidhoofisha_iran
Brigedia Jenerali Amir Hatami, Waziri wa Ulinzi wa Iran leo amesema kuwa maadui wameunga mkono ugaidi katika Mashariki ya Kati na kutekeleza njama za kuzusha machafuko katika nchi za eneo hili ikiwemo huko Iraq, Syria na pia kuidhoofisha Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 04, 2018 10:45 UTC
  • Hatami: Kuwaunga mkono magaidi; njama ya maadui kwa ajili ya kuidhoofisha Iran

Brigedia Jenerali Amir Hatami, Waziri wa Ulinzi wa Iran leo amesema kuwa maadui wameunga mkono ugaidi katika Mashariki ya Kati na kutekeleza njama za kuzusha machafuko katika nchi za eneo hili ikiwemo huko Iraq, Syria na pia kuidhoofisha Iran.

Brigedia Jenerali Hatami amesema kuwa maadui wamejaribu kuyumbisha hali ya usalama na kuzusha machafuko katika eneo hili hata hivyo njama zao zote zimesambaratishwa. Ameshukuru busara za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Sayyid Ali Khamenei na uelewa wa vikosi vya Iran katika medani ya mapambano. Waziri wa Ulinzi wa Iran ameongeza kuwa moja ya nchi za eneo hili imekiri kuwa imetumia dola bilioni 137 kuendesha njama zake ili kuitumbukiza Iran katika machafuko na kuyaunga mkono makundi ya kigaidi huko Iraq na Syria. Amesema Marekani na nchi nyingine pia zimetumia zaidi ya dola bilioni 5000 kuibua machafuko katika Mashariki ya Kati.

Amesema lengo kuu la Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel lilikuwa ni kuasisi ugaidi na makundi ya jinai ili kudhihirisha picha mbovu ya Uislamu iliyochanganyika na machafuko, umwagaji damu na vitendo vya uchupaji mipaka.