Amoli: Walimwengu wameng'amua mienendo ya kindumakuwili ya Marekani kuhusu ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i47735-amoli_walimwengu_wameng'amua_mienendo_ya_kindumakuwili_ya_marekani_kuhusu_ugaidi
Mkuu wa Idara ya Mahakama nchini Iran amesema kuwa, mienendo ya kindumakuwili ya Marekani kuhusiana na jinai zinazofanywa na magaidi imedhihirika waziwazi kwa walimwengu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 28, 2018 03:08 UTC
  • Amoli: Walimwengu wameng'amua mienendo ya kindumakuwili ya Marekani kuhusu ugaidi

Mkuu wa Idara ya Mahakama nchini Iran amesema kuwa, mienendo ya kindumakuwili ya Marekani kuhusiana na jinai zinazofanywa na magaidi imedhihirika waziwazi kwa walimwengu.

Ayatullah Sadiq Amoli Larijani amesema kuwa walimwengu hawawezi kukubali kuona mfumo wa kibeberu ukidai kidhahiri kuwa unapambana na ugaidi na katika upande mwingine unayasaidia kifedha na kisiasa makundi ya kigaidi.

Larijani ameashiria uhusiano mkubwa uliopo baina ya Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Rais wa Marekani John Bolton na kundi la kigaidi la MKO na kusema: Viongozi wa sasa wa Marekani wanashirikiana na makundi ya kigaidi kwa lengo la kutoa dhurba na pigo kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mkuu wa Idara ya Mahakama nchini Iran amezungumzia jinai zilizofanywa na kundi la kigaidi la MKO nchini Iran katika kipindi chote cha miaka 40 iliyopita na kusema kuwa, kundi hilo limeondolewa katika orodha ya makundi ya kigaidi kwa msaada wa Marekani, Ufaransa na Uingereza. 

Kundi la kigaidi la MKO limeua shahidi raia elfu 17 wa Iran likisaidiwa na Marekani, Israel, Uingereza na Ufaransa.