Zarif: Misimamo mikali na ugaidi havina dini wala taifa
-
Muhammad Javad Zarif
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amekemea vikali shambulizi la kigaidi lililolenga hekalu la Kiyahudi la Tree of Life huko Pittsburgh, katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani na kusisitiza kuwa, ukatili na ugaidi havina dini wala mbari na vinapaswa kulaani kwa hali yoyote ile.
Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twetter Muhammad Javad Zarif amelaani shambulizi hilo na kusema: Ulimwengu haupaswi kuishi chini ya wahemshaji wenye silaha.
Vilevile amelitaja shambulizi hilo kuwa ni hujuma ya kigaidi.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran ametoa mkono wa pole na kutuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulizi la hekalu la Kiyahudi la Tree of Life huko Pittsburgh.
Shambulizi hilo lililofanywa na mtu aliyejulikana kwa jina la Robert Bowers, 48, limeua watu wasiopungua 14 na kujeruhi wengine 12. Mtuhumiwa huyo ambaye anashikiliwa na vyombo vya usalama vya Marekani amekiri kuhusika na jinai nyingine 29.
Uchunguizi wa awali unaonesha kuwa alikuwa na ruhusa rasmi ya kumiliki silaha.