Waziri Mkuu wa Italia asisitiza kutekelezwa makubaliano na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i4978-waziri_mkuu_wa_italia_asisitiza_kutekelezwa_makubaliano_na_iran
Waziri Mkuu wa Italia ametilia mkazo kutekelezwa makubaliano yaliyosianiwa kati ya nchi yake na Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 13, 2016 09:46 UTC
  • Waziri Mkuu wa Italia asisitiza kutekelezwa makubaliano na Iran

Waziri Mkuu wa Italia ametilia mkazo kutekelezwa makubaliano yaliyosianiwa kati ya nchi yake na Iran.

Akizungumza hii leo katika kikao cha Kiuchumi kati ya Iran na Ulaya hapa Tehran, Matteo Renzi Waziri Mkuu wa Italia amesisitiza kutekelezwa makubaliano yaliyosainiwa kati ya nchi hiyo na Iran na kuongeza kuwa, Benki ya Ulaya ya Unicredit imesaini hati ya makubaliano na viongozi wa Iran ili kufungua tawi lake nchini Iran.

Kuhuishwa njia ya hariri na kushirikiana katika sekta ya vyakula ni masuala mengine yanayopatiwa kipaumbele maalumu na Italia katika ushirikiano wake na Iran. Matteo Renzi amesema kuwa kuzingatiwa masuala ya kibenki katika kuendeleza ubadilishanaji wa kibiashara na kiuchumi kati ya Iran na Italia, ni miongoni mwa vipaumbele vinavyozingatiwa na nchi yake na Iran.

Waziri Mkuu wa Italia ameashiria pia mazungumzo aliyofanya na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kueleza kuwa, familia hii kubwa inaweza kuasisi jiwe la msingi wa amani duniani.

Wawakilishi wa sekta binafsi ya Italia na wale wa serikali, wawakilishi wa chumba cha kibishara na sekta ya viwanda na madini ya Iran wamesaini makubaliano 12 ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali za nishati, chuma cha pua, mawasiliano, uzalishaji nguvu za umeme, habari, masuala ya viwanja vya ndege na tiba, kwa kuhudhuriwa na Waziri Mkuu wa Italia na Waziri wa Viwanda, Madini na Biashara wa Iran. Matteo Renzi Waziri Mkuu wa Italia jana aliwasili Tehran akiongoza ujumbe wa kisiasa na kiuchumi wa watu 250.