Iran: Ni kupoteza wakati kwa Washington kusubiri kufanya mazungumzo na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55323-iran_ni_kupoteza_wakati_kwa_washington_kusubiri_kufanya_mazungumzo_na_iran
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa ni bure na upuuuzi kwa Washington kuwa na matarajio kwamba, viongozi wa Marekani watafanya mazungumzo ya simu na wa Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 11, 2019 22:13 UTC
  • Iran: Ni kupoteza wakati kwa Washington kusubiri kufanya mazungumzo na Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa ni bure na upuuuzi kwa Washington kuwa na matarajio kwamba, viongozi wa Marekani watafanya mazungumzo ya simu na wa Iran.

Sayyid Abbas Mousavi amesema kuwa viongozi wa Marekani wametangaza kuwa, Rais wa nchi hiyo Donald Trump angali ana matarajio ya kufanya mazungumzo ya simu na viongozi wa Iran na ni kwa muda sasa ambapo Marekani inasubiri kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hata hivyo Iran kamwe haitaketi katika mazungumzo ambayo ndani yake sheria na kanuni za kimataifa zinapuuzwa. 

Rais Donald Trump wa Marekani  
 

Mousavi ameashiria ugaidi wa kiuchumi wa Marekani dhidi ya Iran na kusema kuwa: Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu anayefanya mazungumzo na mtu anayemshinikiza na kuelekeza silaha upande wake. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameendelea kusema kuwa viongozi wa Marekani siku zote wameonesha kwamba si wakweli katika maneno na matamshi yao na katika upande mmoja, wanawawekea vikwazo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na mkuu wa chombo cha diplomasia cha Iran (Waziri wa Mambo ya Nje) na wakati huo huo wanataka kufanya mazungumzo na Iran.  

Mousavi amesisitiza kuwa, viongozi wa Marekani wamechanganyikiwa katika siasa zao za nje.