Mdahalo wa mwisho wa Urais nchini Iran unafanyika leo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i71170-mdahalo_wa_mwisho_wa_urais_nchini_iran_unafanyika_leo
Mdahalo wa tatu na wa mwisho wa wagombea wa urais nchini Iran unafanyika alasiri ya leo mwendo wa saa kumi na moja kwa saa za hapa nchini, kupitia televisheni na radio za taifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 12, 2021 02:42 UTC
  • Mdahalo wa mwisho wa Urais nchini Iran unafanyika leo

Mdahalo wa tatu na wa mwisho wa wagombea wa urais nchini Iran unafanyika alasiri ya leo mwendo wa saa kumi na moja kwa saa za hapa nchini, kupitia televisheni na radio za taifa.

Mdahalo wa leo unatazamiwa kujikita zaidi katika masuala ya madukuduku ya wananachi kuelekea uchaguzi wa rais utakaofanyika Ijumaa ijayo.

Mdahalo wa kwanza ulifanyika Jumamosi  ya Juni 5,  huku wa pili  ukiwa ulifanyika Jumanne ya tarehe  8 Juni.

Wagombea urais katika uchaguzi wa mwaka huu nchini Iran ni Saeed Jalili, Mohsen Rezaee Mirgha'ed, Sayyid Ebrahim Raisi, Alireza Zakani, Sayyid Amir-Hossein Ghazizadeh Hashemi, Mohsen Mehralizadeh na Abdolnaser Hemmati.

Rais wa sasa Hassan Rouhani anakamilisha muhula wake wa pili mfululizo na hivyo haruhusiwi kugombea awamu hii kisheria.

Wagombea urais nchini Iran

Kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini Iran, kampeni za uchaguzi za wagombea wa urais zilianza rasmi tarehe 25 Mei ambapo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran ilitangazwa majina ya wagombea. Kampeni hizo zinaendelea hadi masaa 24 kabla ya kuanza zoezi la kupiga kura.

Wagombea wote nchini Iran wanapewa haki sawa kwa kuhesabiwa mpaka sekunde za kufanya kampeni katika Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, bila ya kupunguziwa au kuongezewa hata sekunde moja. 

Uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na uchaguzi wa 6 wa mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya tarehe 18 mwezi huu wa Juni, 2021.