Uchaguzi wa Rais wa 13 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i71446-uchaguzi_wa_rais_wa_13_wa_jamhuri_ya_kiislamu_ya_iran
Uchaguzi wa Rais wa 13 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulifanyika jana nchini kote Iran kwa kushirikisha idadi kubwa ya wananchi waliotumia haki yao ya kidemokrasia na kumchagua rais wao ajaye.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 19, 2021 08:56 UTC
  • Uchaguzi wa Rais wa 13 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Uchaguzi wa Rais wa 13 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulifanyika jana nchini kote Iran kwa kushirikisha idadi kubwa ya wananchi waliotumia haki yao ya kidemokrasia na kumchagua rais wao ajaye.

Zoezi la kupiga kura lilianza asubuhi saa moja kamili za kumalizika saa nane usiku baada ya kurefushwa muda wake mara tano kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa wakiendelea kupiga kura. Hadi tunatayarisha uchambuzi huu matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais na Mabaraza ya Miji na Vijiji nchini Iran yalikuwa yakionyesha kuwa, Sayyid Ebrahim Raeisi amepata ushindi wa kishindo katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Kiislamu.

Sayyid Ebrahim Raeisi

Uchaguzi wa Rais wa Iran ambao umekuwa ukijadiliwa sana katika duru za kisiasa za ndani na nje ya nchi kwa miezi kadhaa iliyopita umeakisiwa sana katika vyombo vya habari vya kikanda na kimataifa.

Waandishi wa habari wa mashirika kama AFP, Reuters, The New York Times, The Washington Post, Le Monde, Le Fiigaro, Der Spiegel, Zoddeutsche Zeitung, Bild, Austrian Standard, El Pais, France 24, BBC al Jazeera, al Manar na kadhalika yaliakisi moja wa moja na kuripoti matukio ya uchaguzi wa Rais na Mabaraza ya Miji na Vijiji hapa nchini.

Mashirika mengi ya habari kama Reuters, CNN, Associated Press, Xinhua na Sputnik yametangaza kuwa idadi kubwa ya Wairani wameshirki katika zoezi hilo la kuchagua Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ukweli ni kwamba, Ijumaa ya jana ya tarehe 18 Juni Iran ilishuhudia tukio jingine muhimu sana katika historia ya miaka zaidi ya 42 ya Mapinduzi ya Kiislamu. Ayatullah Ali Khamenei ambaye alipiga kura saa moja asubuhi jana Ijumaa katika Husainiya ya Imam Khomeini mjini Tehran alisema siku ya uchaguzi ni siku ya taia la Iran na kuongeza kuwa: Leo wananchi ndio wenye uwanja na medani na kwa kura zao wanaainisha ramani ya nchi kwa ajili ya miaka kadhaa ijayo, hivyo leo ni siku yao. 

Wairan katika uchaguzi wa rais

Mahudhurio makubwa ya Wairani katika uchagzi wa jana wa Rais yametoa ujumbe mbili muhimu:

Ujumbe wa kwanza ni kwamba, umeakisi mtazamo mpana na maono makini ya taia la Iran, kutambua zama na kuwajibika katika vipindi nyeti na muhimu na vilevile uwezo wake wa kuchukua maamuzi sahihi katika wakati mwafaka. Wairani wameshiriki kwa wingi katika zoezi hilo katika kipindi ambacho wamekuwa wakilalamika sana kutokana na matatizo ya kipindi cha sasa kama mfumuko wa bei, ughali wa maisha, ukosefu wa ajira na matatizo mengine ya kiuchumi. Hata hivyo wanaelewa vyema kwamba, ufumbuzi wa maatizo hayo ni kumchagua mtu na kiongozi sahihi na anayefaa na wala si kususia uchaguzi kama walivyotaka wapinzani wa utawala wa Kiislamu na mabeberu wa kimataifa na vibaraka wao.

Ujumbe wa pili wa mahudhurio makubwa ya wananchi wa Iran katika uchaguzi wa jana ni kutimiza msingi wa kushirikishwa wananchi katika kuchuka maamuzi muhimu ya kitaifa, suala ambalo limekuwa likitiliwa mkazo daima tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini.

Hapana shaka kuwa matokeo ya uchaguzi wa jana hapa nchini ni mshikamano wa kisiasa na umoja wa kitaifa na kidini. Matokeo ya uchaguzi huo pia yataanda mazingira ya kushirikishwa nguvu kazi mpya na yenye mitazamo na maono mapya katika kazi mbalimbali na kuwa mwanzo wa harakati mpya ya kuelekea kwenye ufanisi na maendeleo zaidi.

Tajiriba ya chaguzi zaidi ya 38 zilizopita hapa nchini baadaa ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979 inaonesha kuwa, wakati wote ushiriki wa wananchi katika zoezi la kupiga kura unapokuwa mkubwa, huwa na taathira nyingi chanya za kisiasa, kijamii na kiuchumi. Sasa inatupasa kusubiri na kuona rais ajaye wa Iran atatekelza kwa kiwango gani ahadi zake alizotoa kwa wananchi kwenye kampeni zake za uchaguzi.