Kamanda Hajizadeh: Maadui wasithubutu kuijaribu Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i73840-kamanda_hajizadeh_maadui_wasithubutu_kuijaribu_iran
Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema maadui wanafahamu vyema uwezo mkubwa wa Iran na irada ya taifa hili la Kiislamu ya kuzima tishio lolote dhidi yake; hivyo hawapaswi kuthubutu kuchukua hatua yoyote ya kuijaribu nchi hii.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 23, 2021 06:54 UTC
  • Kamanda Hajizadeh: Maadui wasithubutu kuijaribu Iran

Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema maadui wanafahamu vyema uwezo mkubwa wa Iran na irada ya taifa hili la Kiislamu ya kuzima tishio lolote dhidi yake; hivyo hawapaswi kuthubutu kuchukua hatua yoyote ya kuijaribu nchi hii.

Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh amenukuliwa akisema hayo na shirika la habari la Fars na kuonya kuwa, Iran haitasita kutoa jibu kali lenye kuumiza kwa hatua yoyote ya kichokozi ya adui. 

Brigedia Jenerali Hajizadeh amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni taifa kubwa na lenye uwezo mkubwa, jambo ambalo linawatia kiwewe maadui.

Amebainisha kuwa, "iwapo kutatokea uvamizi wowote dhidi ya Iran, hakuna shaka kuwa jibu la Jamhuri ya Kiislamu kwa uchokozi wa maadui litakuwa kali, na kwa msingi huo hawapaswi kufanya kosa hilo la kimahesabu."

Uwezo wa makombora wa Iran

Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza bayana kuwa, Iran imepiga hatua kubwa ya kujitosheleza katika uga wa ulinzi, na hii ni stratejia ya ushindi iliyochukuliwa na Iran dhidi ya madola ya kibeberu.

Jenerali Hajizadeh ameongeza kuwa, motisha na ari ya juu ya vikosi vya ulinzi vya Ira imelifanya taifa hili lipate mafanikio mengi, chini ya miongozo na maelekezo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapindizi ya Kiislamu, Ayatulah Sayyid Ali Khamenei.