Watu wengine 709 wameaga dunia nchini Iran kwa ugonjwa wa Covid-19
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i73878-watu_wengine_709_wameaga_dunia_nchini_iran_kwa_ugonjwa_wa_covid_19
Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran imetangaza kuwa, watu 709 wameaga dunia hapa nchini katika saa 24 zilizopita kutokana na ugonjwa wa Covid-19.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 24, 2021 08:37 UTC
  • Watu wengine 709 wameaga dunia nchini Iran kwa ugonjwa wa Covid-19

Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran imetangaza kuwa, watu 709 wameaga dunia hapa nchini katika saa 24 zilizopita kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Kituo cha habari na mawasiliano ya umma cha Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran kimetangaza leo kuwa, wagonjwa 709 wamefariki dunia katika muda wa saa 24 zilizopita kutokana na maambukizo ya virusi vya corona na kuifanya idadi ya watu wote waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Covid-19 hapa nchini kufikia 103,357.

Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran imetangaza pia kuwa, kwa mujibu wa matokeo ya vipimo rasmi, katika muda wa masaa 24 yaliyopita wagonjwa wapya 40,623 waliokumbwa na ugonjwa wa COVID-19 wamegunduliwa humu nchini, na kuifanya idadi ya watu wote waliobainika kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo kufikia 4,756,394.

Kwa mujibu wa ripoti ya wizara hiyo, hadi sasa wagonjwa 3,993,211 wamepata afueni na kuruhusiwa kutoka hospitali na kurejea majumbani.

Wakati huohuo Wizara ya Afya ya Iran imetangaza kuwa watu 17,233,661 wameshapatiwa dozi ya kwanza ya chanjo ya Covid-19 na wengine 6,476,773 wameshapokea dozi ya pili ya chanjo ya ugonjwa huo na kuifanya idadi ya chanjo zilizotolewa hapa nchini hadi sasa kufikia dozi 23,710,434.../