Mkuu wa timu ya mazungumzo ya Iran arejea Vienna
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i81212-mkuu_wa_timu_ya_mazungumzo_ya_iran_arejea_vienna
Mkuu wa timu ya mazungumzo ya Iran amerejea Vienna mji mkuu wa Austria ili kuendelea na mazungumzo ya nyuklia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 10, 2022 00:41 UTC
  • Mkuu wa timu ya mazungumzo ya Iran arejea Vienna

Mkuu wa timu ya mazungumzo ya Iran amerejea Vienna mji mkuu wa Austria ili kuendelea na mazungumzo ya nyuklia.

Ali Bagheri Kani ambaye alirejea Tehran kwa lengo la kushauriana na viongozi wa ngazi ya juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, jana asubuhi alielekea Vienna kuendelea na mazungumzo hayo.  

Viongozi wa Iran na wa kundi la 4+1 wamesema kuwa, mazungumzo ya kuhuisha mapatano ya JCPOA yamefika katika hatua ya mwisho, na kwamba pande mbili zinapasa kuchukua maamuzi ya kisiasa kuhusiana na masuala kadhaa yaliyosalia. 

Mijadala na mashauriano yanaendelea katika Hoteli ya kifahari ya Coburg huko Vienna katika fremu ya duru ya 8 ya mazungumzo ya Vienna kati ya Iran na kundi la 4+1 linaloundwa na Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Russia na China pamoja na Mratibu wa Umoja wa Ulaya. 

Mazungumzo kuhusu JCPOA yanaendelea Vienna 

Mazungumzo hayo yamekuwa na mafaniko kutokana na ubunifu wa timu ya mazungumzo ya Iran; hata hivyo kusitasita pande za Magharibi hasa serikali ya Joe Biden kufidia vitendo na hatua zilizo kinyume cha sheria za serikali iliyopita ya Marekani; na wakati huo huo kuendelezwa wenzo wa mashinikizo ya kiwango cha juu, vimepelekea kutiliwa shaka nia ya Marekani iwapo kweli imekusudia kurejea katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA sambamba na kurefusha mchakato wa mazungumzo.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza mara kadhaa kwamba Marekani ndio iliyojitoa katika mapatano ya JCPOA; na kwa msingi huo inapasa kwanza iondoe vikwazo vyake dhidi ya Iran ili iweze kurejea katika mapatano hao na itekeleza majukumu yake na kutoa hakikisho kwamba haitakiuka tena mapatano hayo.