Imam Khomeini alileta taswira sahihi ya Uislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i8386-imam_khomeini_alileta_taswira_sahihi_ya_uislamu
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo ya hapa Tehran amesema, Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini MA, aliisafisha taswira ya Uislamu kutokana na upotoshaji hatari wa Marekani, wa kutenganisha dini na siasa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 03, 2016 09:40 UTC
  • Imam Khomeini alileta taswira sahihi ya Uislamu

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo ya hapa Tehran amesema, Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini MA, aliisafisha taswira ya Uislamu kutokana na upotoshaji hatari wa Marekani, wa kutenganisha dini na siasa.

Hujjatul Islam wal Muslimin Kazem Seddiqi, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran, sambamba na kutoa salamu za rambi rambi kwa mnasaba wa kukumbuka siku ya kuaga dunia Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Imam Khomeini alikuwa faqihi mwenye kuleta ubunifu na kuandika historia.

Ameongeza kuwa, moja ya sifa za kipekee za Imam Khomeini ni kwamba alikuwa kiongozi mwenye hekima na mantiki na hivyo aliweza kuuletea Uislamu heshima na nguvu. Amesema Imam Khomeini aliuhuisha Uislamu sambamba na kuhuisha mapambano dhidi ya udhalimu na ufisadi.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran pia ameashiria kuhusu kuzinduliwa duru nyingine ya Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanamchagua Kiongozi Muadhamu na kuongeza kuwa, kushiriki kwa wingi wananchi wa Iran katika Uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) na Baraza la Wanazuoni Wataalamu ni jambo lililowakasirisha mno maadui.

Hujjatul Islam Kazem Seddiqi ameashiria pia kuanza kazi Bunge la Kumi la Iran na kusema, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anatazamia bunge hili lizingatie uchumi na kuimarisha misingi ya utamaduni wa kidini nchini.