Mtafiti Muirani Ashinda Tuzo ya Dunia ya Kemia mwaka 2016
(last modified Sun, 12 Jun 2016 04:29:43 GMT )
Jun 12, 2016 04:29 UTC
  • Mtafiti Muirani Ashinda Tuzo ya Dunia ya Kemia mwaka 2016

Mtafiti Muirani ameshinda Tuzo ya Kimataifa ya Mwanakemia Bora wa Kijani mwaka 2016.

Dkt. Ali Maliki mhadhiri msaidizi katika Kitivo cha Kemia cha Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Iran ametunukiwa tuzo hiyo na Jumuiya ya Kimataifa ya Kemia.

Dkt. Maliki amepata tuzo hiyo ijulikanayo kama, IUPAC-CHEMRAWN VII for Green Chemistry, kutokana na mchango wake mkubwa katika kemia ya kijani.

Msomi huyo Muirani ameandika makala zaidi ya 120 katika Jarida la Kimatiafa la Kisayanis la ISI mbali na kuwasilisha makumi ya miradi na mipango ya utafiti wa kitaifa yenye muelekeo wa kulinda mazingira.

Hafla ya kumtunuku zawadi mwanakemia hiyo Muirani itafanyika baadaye mwezi Septemba mwaka huu.

Jumuiya ya kimataifa ya Kemia IUPAC hutoa zawadi hiyo mara moja kila miaka miwili ambapo wanaotunukiwa huwa ni wanasayansi vijana wasiozidi umri wa miaka 45 ambao huwa wametia fora zaidi katika harakati za kisayansi katika uga wa kemia ya kijani yenye lengo la kulinda mazingira.

 

Tags