Amir-Abdollahian: Iran iko tayari kuchukua hatua kufikia mapatano ya nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i92058-amir_abdollahian_iran_iko_tayari_kuchukua_hatua_kufikia_mapatano_ya_nyuklia
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuchukua hatua za mwisho za kufikia makubaliano ya nyuklia na kufuta vikwazo vya kidhalimu."
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Dec 24, 2022 03:41 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian
    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuchukua hatua za mwisho za kufikia makubaliano ya nyuklia na kufuta vikwazo vya kidhalimu."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Ijumaa usiku kwamba: "Katika mkutano na Josep Borrell, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, ameafiki kuhusu kuchukuliwa hatua za mwisho za makubaliano ya nyuklia."

"Wakati huo huo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amefafanua kuwa: "Mwanya wa makubaliano ya Iran hautakuwa wazi milele." Aidha ametilia mkazo suluhisho la kisiasa la mgogoro wa Ukraine na kusema Marekani haistahiki kutoa nasaha kwa wengine kutokana na kuhusika kwake na majanga ya Guantanamo na Abu Ghraib, na jinai dhidi ya wanawake na watoto huko Yemen na Afghanistan. Kabla ya kushiriki katika mkutano wa Baghdad-2 huko Amman, mji mkuu wa Jordan, Amir- Abdollahian aliwaambia waandishi wa habari kwamba anaenda kukutana na afisa wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya kando ya mkutano huo.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran alikuwa ameeleza matumaini yake kwamba kwa mujibu wa mkabala wa Wamarekani katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, kutakuwa na mabadiliko katika mtazamo na mienendo ya watawala wa Washington. Amir-Abdollahian amewaeleza wazi Wamarekani kwamba ni lazima wachague moja kati ya unafiki au kutaka mapatano na kuirejesha Marekani kwenye JCPOA. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisafiri Jumanne iliyopita kwenda kushiriki katika mkutano wa Baghdad-2 huko Amman, mji mkuu wa Jordan.

Wiki iliyopita pia Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa alisema iwapo Marekani inataka kweli kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, haina chaguo jingine isipokuwa kukhitari njia ya diplomasia badala ya mashinikizo, vitisho na makabiliano.