Jan 03, 2023 02:16 UTC
  • Hossein Amir-Abdollahian
    Hossein Amir-Abdollahian

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa duru ya nne ya mazungumzo kati ya Iran na Iraq kwa ajili ya kufuatilia faili la mauaji ya Shahidi Qassem Soleimani na wanajihadi wenzake itafanyika Iran.

Shughuli ya kukumbuka kuingia mwaka wa tatu tangu kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani zilianza jana zikihudhuriwa na wanadiplomasia na maafisa wa mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran. 

Mbali na Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Manaibu, Wakurugenzi na wafanyakazi wa wizara hiyo, Brigedia Jenerali Hossein Salami Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na baadhi ya wanadiplomasia wa zamani pia wanashiriki katika shughuli hiyo.  

Hossein Amir-Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisema katika shughuli hiyo iliyofanyika katika jengo la Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kwamba, katika upande wa ushirikiano na serikali ya Iraq hadi sasa kumefanyika duru tatu za mazungumzo ya kiufundi na ya kina na duru ya nne itafanyika hapa Tehran.  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa chombo hicho cha kidiplomasia kina jukumu kuu katika kufuatilia faili la mauaji ya Shahidi Luteni Jenerali Soleimani ambapo kamati maalumu imeundwa katika Wizara ya Mambo ya Nje kwa kushirikiana kwa karibu na Idara ya Mahakama na Jeshi la Sepah. 

Lt. Jenerali Soleimani, ambaye alikuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Naibu Kamanda Jeshi la Kujitolea la Wannachi wa Iraq (PMU) Abu Mahdi al-Muhandis, na wanamapambano wenzao waliuawa shahidi katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mapema  Januari 3, 2020. Shahidi Soleimani alikuwa ameelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo.

Tags