Jan 03, 2023 03:04 UTC
  • IRGC: Kulipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Shahidi Soleimani ni jambo lisilo na shaka

Katika mwaka wa tatu wa kuuawa shahidi Jenerali Hajj Qassem Soleimani, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesema kulipiza kisasi dhidi ya wahalifu na wauaji wa shahidi huyo ni jambo ambalo bila shaka litafanyika.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), aliuawa shahidi katika shambulio la anga la jeshi vamizi la Marekani Januari 3, 2020, akiwa safarini nchini Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, Vikosi vya jeshi la kigaidi vya Marekani vilitekeleza hujuma hiyo katika uwanja wa ndege wa Baghdad ambapo Shahid Soleimani aliuawa akiwa pamoja na Abu Mahdi Al-Muhandis, aliyekuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq pamoja na wanamapambano wengine 8 waliokuwa wameandamana nao.

Taarifa ya IRGC imeeleza kuwa mauaji ya Jenerali Haj Qassem Soleimani, yalikuwa ya kidhalimu  na kwamba jina, kumbukumbu, maadili na ubunifu mkubwa wa kamanda huyo wa muqawama katika eneo la Asia Magharibi, limeenea katika kona zote za dunia miongoni mwa walimwengu hususan vizazi vya vijana na Mujahidina waaminifu wanaotafuta uadilifu na mapambano dhidi ya udhalimu katika pembe zote za dunia.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: Shahidi Haj Qassem Soleimani, kutokana na imani yake, unyoofu, ari, utashi, ujasiri, hatua ya kimapinduzi na imani ya kina, alikuwa shujaa na bingwa wa kudumu wa Iran na Wairani, na shujaa wa ulimwengu katika mapambano dhidi ya Wazayuni na uistikbari wa kimataifa.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa kuzuiwa fitna za Daesh katika eneo na usalama thabiti wa Iran leo ni mambo yaliyopatikana kutokana na juhudi kubwa na za kujitolea za Haj Qasim na watetezi wa Haram na yanachukuliwa kuwa nguzo za kuzuia na mdhamini wa usalama wa nchi.

Hali kadhalika taarifa hiyo imesisitiza kuhusu uimara wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Quds katika kuendeleza stratijia ya kuunga mkono Mapambano ya Kiislamu kama kielelezo cha kuendelea na njia ya Jenerali Soleimani na kubakia kwenye malengo bora ya taifa la Iran na uungaji mkono wa taifa la Palestina na ukombozi wa Quds Tukufu.

Tags