Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhutubia Mkutano wa Wakuu Jumuiya ya Shanghai
(last modified 2023-07-04T04:35:03+00:00 )
Jul 04, 2023 04:35 UTC
  • Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhutubia Mkutano wa Wakuu Jumuiya ya Shanghai

Rais wa Iran ambaye ni miongoni mwa wanachama wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran atahutubia Mkutano wa 23 wa Wakuu wa jumuiya hiyo utakaofanyika kwa njia ya intaneti huko New Delhi.

Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Iran kwa mara ya kwanza akiwa mwanachama mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai leo Jumanne atabainisha mitazamo na misimamo ya Iran katika Mkutano huo utakaofanyika kwa njia ya intaneti huko New Delhi mji mkuu wa India.  

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikuwa mwanachama mtazamaji tokea mwaka 2005; ambapo ombi la kwanza la kutaka kupatiwa uanachama rasmi na kamili ndani ya jumuiya hiyo pia baada ya miaka 16 liliidhinishwa mwaka 2021 katika Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai uliofanyika huko Dunshabe mji mkuu wa Tajikistan.

Iran imekuwa mwanachama wa tisa wa jumuiya hiyo muhimu ya kikanda baada ya ombi lake kupasishwa na nchi nane wanachama wengine wa Shanghai. Aidha hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kushiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Shanghai. 

Iran mwanachama rasmi ndani ya Jumuiya ya Shanghai 

Moja ya ajenda kuu za Mkutano wa 23 wa Wakuu wa Shanghai ambao unafanyika huko New Delhi kwa uwenyeji wa India kwa njia ya intaneti baada ya kukamilika mchakato wa Iran wa kuwa mwanachama kamili katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ni kutangaza uanachama rasmi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Jumuiya hiyo.

Tags