-
Mamilioni ya Wairani washiriki maandamano ya kitaifa kulaani ghasia zinazoungwa mkono na Marekani, Israel
Jan 12, 2026 06:45Wairani kutoka makundi yote ya jamii wameanza maandamano ya kitaifa kulaani ghasia za karibuni zinazodaiwa kuungwa mkono na mataifa ya nje, wakionesha mshikamano wao na Jamhuri ya Kiislamu.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Hakuna taifa linaloweza kuvumilia ugaidi dhidi ya raia wake na majeshi yake
Jan 12, 2026 06:43Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran, Abbas Araghchi, amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yanayochochewa na Marekani na Israel, ambayo yamekuwa yakiwalenga raia wa Iran pamoja na vikosi vya usalama. Amesisitiza kuwa hakuna nchi inayoweza kufumbia macho ukatili wa aina hiyo, ambao unavunja misingi ya utu na utulivu wa taifa.
-
IRGC yalaani uingiliaji wa wazi wa Trump katika masuala ya ndani ya Iran
Jan 12, 2026 06:41Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limelaani vikali ugaidi wa hivi karibuni katika ghasi za Iran sambam,ba na kumkosoa vikali Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kuingia mausala ya ndani ya Iran.
-
Iran yatangaza siku tatu za kuwaomboleza waliouawa shahidi katika jinai zilizochochewa na US na Israel
Jan 12, 2026 03:09Serikali ya Iran imetangaza siku tatu za maombolezo kwa ajili ya kuwakumbuka waathiriwa, wakiwemo askari wa vikosi vya usalama na wa jeshi la kujitolea, ambao wameuliwa shahidi na wafanyaji fujo na vurugu wanaoungwa mkono na Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel, waliojaribu kuteka nyara maandamano ya amani ya wananchi ya kulalamikia hali ya uchumi nchini.
-
Araghchi: Kuna ushahidi unaowahusisha magaidi wa Mossad na vurugu za mauaji zilizofanywa Iran
Jan 12, 2026 03:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi amesema, kuna ushahidi wa wazi unaohusisha vurugu za mauaji zilizofanywa hapa nchini na magaidi wenye mfungamano na shirika la ujasusi la utawala wa kizayuni wa Israel, Mossad.
-
Pezeshkian: Waliofanya fujo na machafuko Iran si wananchi; ni magaidi kutoka nje
Jan 11, 2026 23:45Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, adui amewaingiza Iran magaidi waliopewa mafunzo maalumu ya kigaidi ili kufanikisha malengo yake na kwamba waliofanya fujo, machafuko na uharibifu katika kona mbalimbali za Iran, si katika wananchi waliokuwa wanaandamana.
-
Baraza la Kulinda Katiba la Iran laitaka polisi kuchukua hatua kali dhidi ya wanaoibua ghasia
Jan 11, 2026 23:44Baraza la Kulinda Katiba la Iran limelaani vikali waibua ghasia na fujo ambao wameharibu mali za umma na kuvunjia heshima misikiti katika maeneo mbalimbali ya nchi, likizitaka taasisi za usalama na mamlaka husika kuchukua hatua zote muhimu kurejesha utulivu na sheria kufuatia matukio ya vurugu.
-
Kwa nini wananchi wa Iran hawana imani na vyombo vya habari vyenye uadui na Jamhuri ya Kiislamu?
Jan 11, 2026 23:10Wananchi wa Iran walio macho na ambao siku zote hujitokeza kwenye medani za harakati, kwa mara nyingine tena wamezima kwa umakini malengo maovu na njama chafu zilizoongozwa kwa ushirikiano wa utawala wa kizayuni na Marekani kupitia vyombo vya habari vyenye uadui na taifa hili.
-
Qalibaf: Iran hivi sasa inapigana vita na adui katika pande 4
Jan 11, 2026 07:28Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa: Leo tunapigana vita na adui wa Kizayuni na Marekani katika pande nne za kiuchumi, kiuelewa, kijeshi na kigaidi.
-
Waziri Araghchi aanika nafasi ya Marekani, Israel katika ghasia za Iran
Jan 11, 2026 03:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amezionya vikali Marekani na utawala haramu wa Israel juu ya matokeo mabaya ya uchochezi na uungaji mkono wao kwa wafanya fujo na wazua rabsha hapa nchini, akisisitiza kuwa Washington na Tel Aviv zinataka kuyageuza maandamano ya kiuchumi ya wananchi wa Iran kuwa machafuko na ghasia.