-
Russia: Hakuna mazungumzo ya kusitisha mapigano mkesha wa Mwaka Mpya
Dec 03, 2025 03:06Msemaji wa Ikulu ya Russia, Kremlin, amesema kuwa, hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kuhusu kusimamishwa vita wakati wa mkesha wa X-Mass na mwaka mpya huko Ukraine.
-
Mapigano yashadidi DRC, kila upande unamtuhumu mwenzake
Dec 03, 2025 03:05Mapigano yamezidi kupamba moto mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku jeshi na waasi wa M23 kila upande ukimshutumu mwenzake kwa kukanyaga makubaliano ya kusitisha mapigano.
-
Putin: Tuko tayari kupigana na Ulaya kama itataka vita
Dec 02, 2025 23:47Rais wa Russia, Vladimir Putin, ameishambulia vikali Ulaya katika matamshi yake ya jana Jumanne, akitangaza utayarifu wa nchi yake kupigana vita dhidi Ulaya, anayoituhumu kuwa inafanya jitihada za kuharibu makubaliano ya kusimamisha mapigano nchini Ukraine na kuishinda Russia kistratijia.
-
Maduro aapa Venezuela haitakubali "amani ya utumwa" ya Marekani
Dec 02, 2025 23:20Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, amesema Caracas haitainama mbele ya shinikizo la kijeshi na kisiasa kutoka Washington, akisisitiza taifa hilo linapinga aina yoyote ya amani ambayo ni sawa na "utumwa" kwa Marekani.
-
UNHCR: Watu 100,000 wamekimbia Kaskazini mwa Msumbiji huku machafuko yakishadidi
Dec 02, 2025 23:18Watu takribani 100,000 wamelazimika kuyakimbia makazi yao kaskazini mwa Msumbiji ndani ya wiki mbili pekee. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Jumanne ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, ambalo limeonya juu ya mashambulizi kuongezeka na kuyakumba maeneo ambayo hapo awali yalikuwa salama, na hivyo kuongeza mzigo wa wahudumu wa kibinadamu waliokwisha elemewa.
-
WHO yaafiki matumizi ya dawa za kupunguza uzito, utipwatupwa ni ugonjwa sugu
Dec 02, 2025 23:17Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limetoa mwongozo wake wa kwanza kuhusu matumizi ya kundi jipya la dawa za kupunguza uzito, hatua inayowakilisha mabadiliko makubwa katika sera za afya duniani wakati viwango vya unene wa kupitiliza au utipwatupwa vikizidi kuongezeka.
-
Wakuu wa ECOWAS wazuru Guinea-Bissau baada ya mapinduzi ya kijeshi
Dec 02, 2025 23:08Ujumbe wa upatanishi wa ngazi ya juu kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ulifanya mkutano Jumatatu na viongozi wa mpito wa Guinea-Bissau kujadili njia ya amani ya kumaliza mgogoro wa kisiasa uliosababishwa na mapinduzi ya kijeshi ya wiki iliyopita.
-
Utajiri wa madini ya Yemen na jicho la tamaa la madola ya kibeberu
Dec 02, 2025 22:52Yemen imegundua utajiri mkubwa wa rasilimali za madini, ikiwa ni pamoja na akiba kubwa ya dhahabu, chuma, titani na madini ya viwandani. Rasilimali hizi zinaweza kufungua njia ya maendeleo ya kiuchumi na kuimarisha nafasi ya kimkakati ya Yemen katika eneo hili zima.
-
Qalibaf: Manuva ya Sahand 2025 ni ishara ya nguvu ya mataifa huru dhidi ya madola ya kibeberu
Dec 02, 2025 09:56Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya iran amesema kuwa, manuva ya kupambana na ugaidi ya Sahand 2025 ni ishara ya nguvu ya mataifa huru dhidi ya madola ya kibeberu.
-
Rais Samia: Vurugu za uchaguzi zililenga kuiangusha serikali
Dec 02, 2025 09:54Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefichua kuwa vurugu za uchaguzi wa Oktoba 29 ziliratibiwa na watu wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuibomoa serikali, na kuzionya vikali taasisi za dini.