Dec 07, 2023 05:01 UTC
  • Wazayuni wakiri kuwa Marekani inashiriki kivitendo katika mauaji ya watu wa Gaza

Wizara ya Vita ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel imekiri katika taarifa kwamba utawala huo umepokea tani 10,000 za zana za kivita kutoka Marekani tangu ulipoanzisha vita dhidi ya watu wa Gaza mnamo tarehe 10 Oktoba.

Kwa mujibu wa televisheni ya Al Jazeera, katika taarifa yake hiyo, wizara ya vita ya utawala wa Kizayuni imeongezea kueleza katika taarifa hiyo kwamba, ndege ya Marekani nambari 200 iliyobeba silaha na zana za kijeshi na magari ya kivita ya Marekani imewasili katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Mapema kabla ya taarifa hiyo, John Kirby, msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa la Ikulu ya White House, alisema katika mahojiano na kituo cha TV cha MSNBC kwamba: "misaada ya kiusalama ya Marekani kwa Israel inaendelea kila siku."

Kirby amefafanua kwa kusema: "sisi tunaendelea kuimarisha uwepo wetu kwa upande wa vikosi vya wanamaji katika eneo ili kutuma ishara kali ya kuzuia mashambulio, kwa upande wowote ambao yumkini utataka kupanua mapigano".

Kwa upande mwingine, Pentagon (Wizara ya Ulinzi ya Marekani) iliwahi kutangaza katikati ya Novemba kwamba makumi ya makomandoo wa Marekani wako huko Israel.

Kulingana na vyombo vya habari, Christopher P. Maier, afisa wa wizara ya ulinzi ya Marekani, amekataa kueleza idadi ya askari wa Marekani wa vikosi vya operesheni maalumuza walioko Israel; lakini maafisa wengine wa Washington wanasema, katika wiki hivi za karibuni, Pentagon imepeleka makumi ya makomandoo kwenye ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kwa kisingizio hicho.../

Tags