Dec 29, 2023 07:07 UTC
  • VIDEO: Askari Mzayuni akiri kuwaua makusudi watoto wa Kipalestina Gaza na anasaka mtoto mchanga pia ili amuue

Askari mmoja wa jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel amekiri kwa fahari kuwa anamsaka mtoto mchanga wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza ili amuue.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) mitandao ya kijamii imesambaza vidio inayomuonyesha mwanajeshi wa Kizayuni ambaye anakiri katika mazungumzo aliyofanya na familia yake kwa kusema: "tunajitahidi kuwatafuta watoto ili tuwaue. Mimi nimefanikiwa kumuua msichana mmoja tu wa miaka 12, lakini ningali ninatafuta mtoto mchanga ili nimuue".

Mashambulio ya kinyama na kikatili yanayoendelea kufanywa na jeshi la utawala dhalimu wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza yamekabiliwa na hisia kali za upinzani na ukosoaji za watu wa pembe mbalimbali za dunia na katika eneo hili, lakini hadi sasa taasisi za kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa bado hazijaweza kuzima na kukomesha mashambulizi hayo.

Itakumbukwa kuwa tarehe 7 Oktoba 2023, makundi ya Muqawama ya Palestina yalianzisha operesheni ya mashambulio ya Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Ukanda Gaza dhidi ya vituo na ngome za utawala wa Kizayuni; na katika hatua ya kulipiza kisasi, kufidia kushindwa kwake na kutaka kusimamisha operesheni za makundi ya Muqawama, utawala huo ghasibu ukaanzisha mashambulio ya kinyama dhidi ya maeneo ya makazi na vituo vya tiba na kiutamaduni vya Ukanda wa Gaza, mashambulio ambayo hadi sasa yamepelekea kuuawa shahidi zaidi ya Wapalestina 21,000 na kujeruhiwa wengine zaidi ya 55,000.

Akthari ya waliouawa katika mashambulio hayo ya mauaji ya kimbari yanayofanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel huko Ukanda wa Gaza mbele ya macho ya walimwengu ni wanawake na watoto.../