Feb 25, 2024 02:27 UTC
  • Kuvunjwa UNRWA; Mpango wa upotoshaji wa Netanyahu kwa ajili ya kuepa kushindwa

Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amewasilisha kwa kile kilichotajwa kama Baraza la Mawaziri la Usalama la utawala huo mpango wa kulivunja Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) ili kuepa taathira za kushindwa mbele ya makundi ya muqawama ya Palestina katika kipindi baada ya vita.

Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni amewasilisha hati na mpango kuhusu zama za baada ya vita katika Ukanda wa Gaza kwa Baraza la Mawaziri la utawala huo. Hati hiyo ya Netanyahu inajumuisha kulivunja Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) na badala yake kuingizwa mashirika mengine ya misaada ya kibinadamu ya kimataifa.  

Mpango huo pia unajumuisha kuanzisha ukanda eti wa usalama huko Ukanda wa Gaza katika maeneo ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na vile vile kufungwa kwa mpaka wa kusini wa Ukanda wa Gaza na Misri. 

Kulingana na mpango huu tajwa ambao Netanyahu ameuwasilisha kwa  Baraza la Mawaziri la Usalama; Israel haitaruhusu kujengwa upya kwa Ukanda wa Gaza hadi eneo hilo litakapopokonywa silaha. Mipango ya ujenzi mpya wa Gaza itatekelezwa kwa kuzingatia mpango wa Netanyahu kwa bajeti na uongozi wa nchi zinazokubaliwa na utawala wa Kizayuni.

Mpango huo wa Netanyahu umewasilisha huku maandamano yakiendelea kushuhudiwa katika mitaa ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel), na familia za mateka wa jeshi la utawala wa Kizayuni zikimtuhumu Netanyahu kuwa ameshindwa kufanikisha kuachiwa huru ndugu zao. Wakati huo huo vyama vinavyoupinga utawala wa Kizayuni ndani ya bunge la utawala huo (Knesset) pia vimetilia mkazo kushtakiwa Baraza la Mawaziri la sasa la utawala wa Kizayuni na kufanyika uchaguzi.  

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel 

Baraza la mawaziri la Netanyahu limekata tamaa tangu kuanza kwa operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa tarehe 7 Oktoba mwaka jana na kushindwa mtawalia jeshi la Kizayuni mbele ya makundi ya muqawama ya Palestina. Netanyahu alikuwa ameahidi ushindi wa haraka dhidi ya makundi ya  Palestina na harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) na kuhitimisha haraka vita na kuudhibiti kikamilifu Ukanda wa Gaza katika hali ambayo katika wiki za karibuni Wazayuni wameshindwa  mtawalia vitani na makundi ya Wapalestina ambapo viongozi wenyewe wa utawala huo wamekiri wazi juu ya suala hilo. 

Mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza 

Katika uga wa kimataifa, uungaji mkono wa pande zote wa Marekani na serikali za Magharibi kwa utawala wa Kizayuni haukuwasaidia viongozi wa  utawala huo ghasibu; na katika upande wa fikra za waliowengi duniani Israel inatambulika kama  utawala unaotenda jinai na unaouwa wanawake na watoto wa Kipalestina. Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imezitaja jinai za utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza katika vikao ilivyoendesha kufuatia mashtaka yaliyowasilisha na mawakilii wa Afrika Kusini kuwa ni mauaji ya kimbari.

Hii ni katika hali ambayo Mamlaka ya Ndani ya Palestina pia imepinga mpango huo wa upotoshoji wa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa eti Gaza baada ya kipindi cha vita. 

Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetangaza kuwa: Mpango wa Netanyahu ni sawa na kutambua rasmi kukaliwa upya kwa mabavu Ukanda wa Gaza na nakuipa Israel mamlaka ya kulidhibiti eneo hilo; jambo ambalo tunalipinga vikali." 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina pia imetangaza kuwa: Mpango wa Netanyahu ni jaribio la kupata muda zaidi wa utekelezaji wa mkakati wa kuwahamisha Wapalestina. 

Mipango ya propaganda na malengo ya kisiasa ya viongozi wa utawala wa Kizayuni katika miaka ya karibuni yamezidisha tu matatizo na vizuizi dhidi ya wakazi wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Gaza. Makundi ya muqawama ya Palestina yanafahamu vyema na yamejianda kukabiliana na na njama na mipango miovu ya viongozi wa utawala ghasibu wa Kizayuni  kwa  azma yao thabiti ya kuendeleza mapambano dhidi ya maghasibu; na katika njia hiyo kumeshuhudiwa umoja na mshikamano kati ya Gaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan. 

Tags