Jeshi la Israel lawaua shahidi Wapalestina 4 Gaza, Ukingo wa Magharibi
Wanajeshi vamizi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewaua shahidi Wapalestina wanne katika mashambulizi mawili tofauti katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza.
Maafisa wa Wizara ya Afya ya Palestina wamesema watu tatu waliuawa shahidi jana Jumanne katika shambulizi la askari makatili wa Israel katika kambi ya wakimbizi ya Jenin, eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Wamesema Wapalestina wengine wasiopungua 20 wamejeruhiwa kwenye hujuma hiyo. Hata hivyo hawataja majina ya Wapalestina waliouawa shahidi katika hujuma hiyo.
Wakati huohuo, askari hao wa Kizayuni wamemuua shahidi kwa kumpoiga risasi kijana mwingine wa Kipalestina aliyekuwa na umri wa miaka 25.
Habari zaidi zinasema kuwa, Yousef Salem Radwan aliuawa jana kwa kupigwa risasi kichwani katika uzio wa mpaka wa Khan Yunis, katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa na Wazayuni maghasibu.
Aidha Wapalestina wengine tisa wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo, ambapo mmoja ameripotiwa kuwa katika hali mbaya kutokana na majeraha ya risasi.
Wimbi hilo la ukatili wa wanajeshi wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi limejiri wakati huu ambapo Wapalestina wameendelea kuandamana katika mpaka wa Gaza kulaani jinai za Wazayuni, kuendelea kuzuiliwa Wapalestina kinyume cha sheria, na kuuvunjia heshima Msikiti Mtukufu wa al-Aqsa.