Wanajeshi wa Kizayuni wanazishambulia timu za matabibu na huduma ya kwanza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103336-wanajeshi_wa_kizayuni_wanazishambulia_timu_za_matabibu_na_huduma_ya_kwanza
Msemaji wa Wizara ya Afya katika Ukanda wa Ghaza ameeleza kuwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wanazishambulia kwa makusudi timu za matabibu wa huduma za kwanza na magari ya kubebea wagonjwa (Ambulances).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 11, 2023 04:41 UTC
  • Wanajeshi wa Kizayuni wanazishambulia timu za matabibu na huduma ya kwanza

Msemaji wa Wizara ya Afya katika Ukanda wa Ghaza ameeleza kuwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wanazishambulia kwa makusudi timu za matabibu wa huduma za kwanza na magari ya kubebea wagonjwa (Ambulances).

Wanamapambano wa Palestina tangu tarehe 7 mwezi huu Oktoba wameanzisha oparesheni ya pande zote na ya aina yake kwa jina la "Kimbunga cha al Aqsa" kutokea Ukanda wa Ghaza kusini mwa Palestina dhidi ya maeneo ya utawala wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.  

Katika muda wa dakika 20 tu, wanamuqawama wa Palestina walivurumisha roketi 5,000 katika maeneo ya Wazayuni na wakat huo huo Hamas wamerusha maparashuti katika anga ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na hivyo kuibua hofu kubwa miongoni mwa Wazayuni maghasibu.  

Wakati huo huo Ashraf Qadra Msemaji wa Wizara ya Afya katika Ukanda wa Ghaza ameeleza kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni mbali na kushambulia maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Ghaza wanazishambulia pia timu za madaktari na wafanyakazi wa huduma ya kwanza, vituo vya afya na pia magari ya kubebea wagonjwa. 

Ashraf Qadra 

Al Qadra ameongeza kuwa, wafanyakazi wa huduma ya kwanza wanafanya kazi katika mazingira hatari na yasiyo na usalama na wanasisitiza kutekeleza majukumu yao mkabala wa raia wa Palestina licha ya hali ngumu wanayopitia.