Hizbullah yazindua kombora jipya katika shambulio dhidi jeshi la Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i111718-hizbullah_yazindua_kombora_jipya_katika_shambulio_dhidi_jeshi_la_israel
Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imetumia kwa mara ya kwanza kombora zito kushambulia eneo la kijeshi la Israel katika sehemu ya kaskazini ya maeneo yaliyokaliwa kwa mabavu mwaka 1948 kwa ajili ya kulipiza kisasi vita vya umwagaji damu vya Israel dhidi ya Gaza.
(last modified 2024-05-13T08:05:14+00:00 )
May 13, 2024 08:05 UTC
  • Hizbullah yazindua kombora jipya katika shambulio dhidi jeshi la Israel

Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imetumia kwa mara ya kwanza kombora zito kushambulia eneo la kijeshi la Israel katika sehemu ya kaskazini ya maeneo yaliyokaliwa kwa mabavu mwaka 1948 kwa ajili ya kulipiza kisasi vita vya umwagaji damu vya Israel dhidi ya Gaza.

Hizbullah imesema katika taarifa fupi kwamba imerusha makombora kadhaa ya yaliyopewa jina la Jihad Mughniyeh, jina la mpiganaji wa kundi hilo ambaye aliuawa shahidi mwaka 2015 katika operesheni nchini Syria ambayo ilihusishwa na Israel. Kombora hilo lililenga mkusanyiko wa wanajeshi wa Israel karibu na eneo la Zebdine huko katika Mashamba ya Shebaa ya Lebanon siku ya Jumapili.

Mughniyeh alikuwa mwanae Imad Mughniyeh, kamanda mwandamizi wa Hizbullah ambaye aliuawa huko Damascus mnamo 2008.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa makombora hayo yalilenga kwa usasisi shabaha zilizokusudiwa na kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo hilo.

Awali, wapiganaji wa muqawama wa Lebanon walilenga kwa kombora gari la kijeshi la Israel, ambalo lilikuwa na vifaa vya ujasusi.

Utawala ghasibu  wa Israel umekuwa ukifanya mashambulizi ya mara kwa mara kusini mwa Lebanon tangu tarehe 7 Oktoba.