MSF watahadharisha kuhusu hali inayozidi kuwa mbaya ya binadamu huko Rafah
Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) imesema kuwa hali ya mji wa Rafah huko kusini mwa Ukanda wa Gaza ni mbaya.
Jumuiya hiyo imeeleza wasiwasi wakke kuhusu hali mbaya ya mji wa Rafah katika Ukanda wa Gaza na kutahadharisha kuwa, akiba ya mahitaji muhimu ya wakazi wa mji huo inakaribia kuisha.
Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) imeendelea kueleza kuwa, vifaa tiba vinakaribia kuisha na kwamba kupungua kwa mafuta kunapelekea kutofanya kazi ipasavyo jenereta na vyanzo vya usambazaji maji safi kwa wakazi wa mji huo.
Uongozi wa Hospitali ya Al Hilal huko magharibi mwa mji wa Rafah pia umetangaza kuwa vitengo mbalimbali vya hospitali hiyo zimejiandaa kupokea majeruhi.
Baraza la mawaziri la vita la utawala wa Kizayuni wa Israel Jumatatu tarehe 6 mwezi huu liliidhinisha mashambulizi ya nchi kavu katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza na jeshi la utawala huo haramu lilianza kuushambulia mji huo siku ya Jumanne licha ya upinzani wa jamii ya kimataifa.
Tangu tarehe 6 mwezi huu hadi sasa utawala wa Kizayuni haujapata mafanikio yoyote zaidi ya kufanya mauaji, uharibifu, jinai za kivita, kukiuka sheria za kimataifa, kuyashambulia mashirika ya misaada ya kibinadamu na kuwasababishia njaa watu wa eneo hilo.