Sababu za kushindwa mazungumzo ya kusitishwa vita vya Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i111736-sababu_za_kushindwa_mazungumzo_ya_kusitishwa_vita_vya_gaza
Khalil al-Hayya, Naibu Mkuu wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, amefafanua jinsi utawala wa Kizayuni wa Israel ulivyovuruga mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza na kubadilishana mateka.
(last modified 2024-05-14T00:08:01+00:00 )
May 14, 2024 00:08 UTC
  • Sababu za kushindwa mazungumzo ya kusitishwa vita vya Gaza

Khalil al-Hayya, Naibu Mkuu wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, amefafanua jinsi utawala wa Kizayuni wa Israel ulivyovuruga mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza na kubadilishana mateka.

Amesema mapendekezo yote yaliyowasilishwa na Hamas yalipuuzwa na kutupiliwa mbali kutokana na vizuizi vya Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala huo wa kibaguzi. Mwezi wa nane wa vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza pia unakaribia kumalizika. Katika mwezi uliopita, jitihada za upatanishi ziliongezeka, ambapo nchi za Misri na Qatar zilijaribu kuipatanisha Hamas na utawala wa Kizayuni. Pamoja na hayo, mazungumzo hayakuwa na matokeo yoyote na yalishindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa. Sababu kadhaa ndizo zilizopelekea kufeli kwa mazungumzo hayo.

Sababu ya kwanza ni kuwa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni anaamini kuwa kuendelea vita ndiko kutafanikisha malengo yake ya kisiasa na si mazungumzo.

Khalil al-Hayya, anasisitiza suala hilo kwa kusema: "Tunatafuta usitishaji vita wa kudumu na mapatano ya kweli kwa ajili ya kubadilishana mateka, lakini Netanyahu anataka kuendeleza vita ili kufikia malengo yake binafsi ya kikatili na kisiasa.Vikosi katili vinavyokalia kimabavu ardhi za Palestina bado vina hamu ya kuendeleza vita vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza, na hili linaonesha kuwa mazungumzo yoyote kuhusu usitishaji mapigano na kubadilishana mateka yanawekewa vizuizi; kitu ambacho hatutakikubali kabisa."

Sababu ya pili ni kwamba hakuna mantiki ya kuendelea na mazungumzo sambamba na kuanzishwa mapigano mapya. Wakati mazungumzo ya kumaliza vita vya Gaza yakiendelea utawala wa Kizayuni umeanzisha mashambulizi dhidi ya Rafah licha ya kuwepo upinzani mkali wa Jamii ya kimataifa dhidi ya hatua hiyo ya kinyama na isiyozingatia ubinadamu wowote.

Mauaji ya umati ya Wazayuni dhidi ya Wapalestina

Kuhusiana na suala hilo, Harakati ya Hamas imetoa tamko ikisema kwamba uvamizi wa adui Mzayuni dhidi ya Rafah na kuteka kivuko chake mara tu baada ya Hamas kukubaliana na pendekezo la upatanishi kwa ajili ya kusimamisha vita ni ishara ya wazi kuwa wavamizi hao hawataki kufikia makubaliano ya kusimamisha vita. Taarifa ya Hamas ilisema: Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu na wa kimabavu na baraza lake la mawaziri lenye misimamo mikali wametumia mazungumzo kama kisingizio cha kushambulia Rafah, kuteka kivuko chake na kuendeleza vita dhidi ya wananchi wa Palestina, hivyo wanabeba dhima kamili ya kuzuia kufikiwa makubaliano ya kusimamishwa vita.

Sababu ya tatu ya kufeli mazungumzo ni kutokuwepo umoja na maafikiano ndani ya baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni. Wajumbe wa baraza hilo walitofautiana pakubwa juu ya kuendelea vita au kuketi kwenye meza ya mazungumzo. Kuhusiana na hilo, tovuti ya habari ya Wazayuni ya "Walla" ililibebesha lawama baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu kwa kufeli mazungumzo ya kusitisha mapigano na kuandika: "Jeshi linalilaumu baraza la mawaziri kwa kushindwa mazungumzo hayo kwa sababu jambo hilo linahatarisha mafanikio katika medani ya mapigano huko Gaza.

Sababu ya nne ya kutofanikiwa mazungumzo hayo ni kutosalimu amri wanamuqwama wa Harakati ya Hamas mbele ya adui Mzayuni. Kusimama kidete kundi la Hamas dhidi ya malengo ya kidhalimu ya utawala katili na unaoukalia kwa mabavu Al-Quds Tukufu kumekuwa mhimili muhimu sana katika uwanja huo.

Wachambuzi na wataalamu wengi wa kistratijia wa nchi za Magharibi wamekiri kwamba, Hamas si tu kwamba imekwamisha utawala wa Tel Aviv katika kufikia malengo yake katika vita vya Gaza, bali pia wameuweka utawala huo katika hali mgumu kwenye mazungumzo.