Hizbullah yashambulia kambi za kijeshi na vituo vya ujasusi vya Israel
Wapiganaji wa harakati ya ya Hizbullah ya Lebanon wameshambulia zana za kijasusi na mikusanyiko ya wanajeshi wa Israel kwenye vituo vya kijeshi karibu na mpaka wa nchi hiyo na ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu mwaka 1948.
Televisheni ya al-Manar ya Lebanon imeripoti kwamba wapiganaji wa Hizbullah walifanya operesheni hiyo jana Jumapili dhidi ya kambi ya kijeshi ya Israel ya al-Malkia.
Wapiganaji wa Hizbullah pia walishambulia mkusanyiko wa wanajeshi wa Israel katika kambi ya kijeshi ya Jal al-Alam kwa kutumia mizinga.
Wapiganaji wa Hizbullah pia wameshambulia mkusanyiko wa wanajeshi wa Israel katika kambi ya kijeshi ya Jal al-Alam. Vulevile wamelenga na kuharibu kabisa mitambo ya ujasusi ya Israel kwenye kituo cha kijeshi cha Ramia.
Mapema jana Jumapili, Hizbullah ilikuwa imepiga kambi ya jeshi la Israel ya al-Raheb huko kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeapa kuendeleza operesheni zake za kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaoendeleza mauaji ya kimbari huko Palestina katika eneo la Ukanda wa Gaza.