Wimbi la walowezi wa Kizayuni wanaokimbia Israel baada ya vipigo vya Iran (PICHA)
(last modified 2024-10-03T10:49:42+00:00 )
Oct 03, 2024 10:49 UTC
  • Wimbi la walowezi wa Kizayuni wanaokimbia Israel baada ya vipigo vya Iran (PICHA)

Baada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutoa vipigo vikali vya makombora dhidi ya maeneo hassasi ya utawala wa Kizayuni, wimbi la kuakhirishwa safari za ndege za kuingia na kutoka Israel nalo limevunja rekodi huku idadi ya walowezi wa Kizayuni walioamua kukimbia Palestina ikiongezeka sana.

Hata kabla ya hapo pia, mashirika ya ndege ya kimataifa yalikuwa yamesimamisha au kupunguza safari zao za kuelekea Israel baada ya utawala wa Kizayuni kushadidisha mashambulio yake dhidi ya Lebanon ambayo yamepelekea pia kuuawa shahidi kidhulma, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah. Wimbi hilo limefunja rekodi baada ya Iran kuyatwanga kwa makombora baadhi ya maeneo nyeti ya utawala wa Kizayuni katika operesheni ya ulipizaji kisasi ya Ahadi ya Kweli 2.

Hapa chini tumeweka baadhi ya picha zinazoonesha wimbi la walowezi wa Kizayuni wakiwa katika foleni ndefu za kukimbia Palestina.

Wimbi la walowezi wa Kizayuni wanaokimbia ardhi za Palestina
Wimbi la walowezi wa Kizayuni wanaokimbia ardhi za Palestina
Mashirika mengi yamefuta au kuakhirisha safari zao kuelekea na kutoka Israel
Hali si hali Israel, walowezi wa Kizayuni wanazidi kukimbia Palestina

 

Tags