Kuendelea dhuma dhidi ya Waislamu wa Kishia Bahrain
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i13723-kuendelea_dhuma_dhidi_ya_waislamu_wa_kishia_bahrain
Shirika la pamoja la kutetea haki za binadamu na demokrasia la Bahrain na Ujerumani limeripoti kuwa utawala wa Aal Khalifa umewaita kuwasaili maulamaa 70 wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 22, 2016 03:57 UTC
  • Kuendelea dhuma dhidi ya Waislamu wa Kishia Bahrain

Shirika la pamoja la kutetea haki za binadamu na demokrasia la Bahrain na Ujerumani limeripoti kuwa utawala wa Aal Khalifa umewaita kuwasaili maulamaa 70 wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo.

Shirika hilo limesema madai ya utawala wa Aal Khalifa kwamba linaheshimu haki za binadamu ni dhihaka tupu na kubainisha kwamba katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita maafisa wa utawala huo wamewaita kuwasaili na kuwahoji maulamaa 70 wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia, wamewatia nguvuni maulamaa wengine 20, washairi tisa  na zaidi ya wanaharakati 50 wa kisiasa; na kwamba hatua hizo ni ithbati ya ukweli wa taarifa ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu dhulma wanazotendewa Waislamu wa Kishia nchini Bahrain.

Maulamaa wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia, Bahrain

Shirika la pamoja la kutetea haki za binadamu na demokrasia la Bahrain na Ujerumani limeashiria kusailiwa kwa watu waliotiwa nguvuni na kuwashinikiza wasaini hati za masharti  ya kuahidi kwamba hawatoshiriki kwenye mgomo wa kuketi chini wa wananchi katika eneo la al-Diraz na kuongeza kuwa uvunjiaji heshima maulamaa wanamapambano wa Bahrain uliomo kwenye hati hiyo unaonyesha jinsi utawala wa kifalme wa Aal Khalifa ulivyoamua kuendeleza hatua za kuwavunjia heshima shakhsia wa kidini wa Kishia.

Mfalme wa Bahrain, Hamad bin Isa Al Khalifa

Shirika hilo aidha limetoa wito kwa utawala wa Aal Khlifa kusimamisha mara moja mashambulio na hujuma dhidi ya raia wa madhehebu ya Shia, kuheshimu haki zao za kiraia, kisiasa na kijamii na kujiepusha na hatua za kuchochea hitilafu za kimadhehebu nchini humo.../