Feb 25, 2016 16:46 UTC
  • Lavrov amjibu Kerry kuhusu mustakabali wa Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov amesema nchi yake na Marekani hazitofuatilia chaguo jengine kwa ajili ya Syria.

Lavrov ameyasema hayo leo mbele ya waandishi wa habari mjini Moscow na kusisitiza kuwa:"hakutakuwepo na chaguo jengine lolote mbadala. Hakuna mtu yeyote mwenye chaguo hilo".

Matamshi hayo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia yanaonekana kuwa ni jibu kwa matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry kwamba endapo usitishaji vita uliopendekezwa nchini Syria utafeli Washington ina machaguo mengine ambayo imeshayafikiria.

Akizungumza siku ya Jumanne katika kikao cha kamati ya uhusiano wa nje ya Seneti ya Marekani, Kerry aliashiria uwezekano wa nchi hiyo kutumia chaguo la nguvu za kijeshi nchini Syria na kueleza kwamba endapo mapigano yataendelea "itakuwa ni kazi ngumu kuhifadhi umoja wa ardhi ya Syria".../

Tags