Nasrullah azitaka nchi zote ziungane kukabiliana na tishio la Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i21127-nasrullah_azitaka_nchi_zote_ziungane_kukabiliana_na_tishio_la_daesh
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kwa kusema: "Njia pekee iliyoko mbele yetu ni kuulinda ustaarabu wa Kiislamu, eneo na uwepo wetu kwa kukabiliana na ugaidi".
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 10, 2016 03:50 UTC
  • Nasrullah azitaka nchi zote ziungane kukabiliana na tishio la Daesh

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kwa kusema: "Njia pekee iliyoko mbele yetu ni kuulinda ustaarabu wa Kiislamu, eneo na uwepo wetu kwa kukabiliana na ugaidi".

Sayyid Hassan Nasrullah amewahutubu watu wanaojaribu kuzusha fitna na hitilafu baina ya Hizbullah na mirengo ya kisiasa ya Lebanon kwa kusema: Wale wanaochimba kisima cha fitna watatumbukia wenyewe kwenye lindi la fitna zao hizo.

Katibu Mkuu wa harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Lebanon aidha amesema Hizbullah ina uhusiano mzuri sana na Rais Michel Aoun wa nchi hiyo unaotokana na kuaminiana baina ya pande mbili.

Katibu Mkuu wa Hizbullah na Rais Michel Aoun

Sayyid Hassan Nasrullah ametangaza kwa mara nyingine uungaji mkono wake kwa Michel Aoun na kueleza kwamba uvumi wa kuwepo hitilafu kati ya Hizbullah na Rais wa Lebanon hauna msingi wowote.

Nasrullah amekanusha pia kauli za watu wanaodai kwamba hali ya kisiasa ndani ya Lebanon ni ya wasisiwasi na ya mgogoro na kubainisha kwa kusema, Hizbullah na aliyekuwa Spika wa Bunge Nabih Berri hawajakwamisha mchakato wa uundaji serikali, na kimsingi makundi yote ya kisiasa yanafanya juhudi za kuondoa vizuizi vinavyokwamisha suala hilo na kwamba hadi sasa imebakia nafasi moja au mbili tu za Wizara ambazo bado hazijajazwa.

Amesisitiza kuwa serikali inapasa kuundwa haraka iwezekanavyo kwa sababu hilo ni kwa manufaa ya nchi; na pande zote zinapaswa kutoa ushirikiano katika jambo hilo…/