Wanawake wa Saudia waendeleza juhudi za kudai haki zao za msingi
(last modified Thu, 06 Apr 2017 07:30:56 GMT )
Apr 06, 2017 07:30 UTC
  • Wanawake wa Saudia waendeleza juhudi za kudai haki zao za msingi

Wanawake wa Saudi Arabia wameendelea na juhudi za kudai haki zao za kijamii kukiwemo kuendesha magari binafsi, ambapo wameanzisha kampeni maalumu katika uwanja huo.

Katika kampeni hiyo wanawake hao wameeneza video, vipeperushi na picha katika maeneo tofauto ya nchi hiyo, wakiitaka serikali ya kifalme ya nchi hiyo kuwapatia haki hiyo ya kijamii. Sababu ya kuanzishwa kampeni hiyo ni kuwashawishi wanawake kutoogopa kutekeleza shughuli hizo za kijamii ambazo tangu awali zimeainishwa kuwa za wanaume peke yao nchini.

Mmoja wa wanawake wa Saudia akiendeleza harakati hizo

Kwa mujibu wa sheria nchini Saudia, mwanamke hawezi kufanya safari peke yake, kufanya shughuli za kifedha au kwenda kwa daktari bila ruhusa ya mume au mtu wake wa karibu. Mbali na hayo ni kwamba tangu mwaka 1957, wanawake wa Saudia wamenyimwa uhuru wa kuendesha gari ndani ya nchi hiyo, kufuatia amri kali iliyopiga marufuku suala hilo. Katika fremu hiyo mwanamke anayekiuka marufuku ya kuendesha gari nchini Saudia hukabiliwa na adhabu kali kukiwemo kuchapwa viboko.

Hii ni katika hali ambayo mbali na sheria za kimataifa, dini ya Uislamu haimzuii mwanamke kuendesha gari madamu atakuwa amechunga mipaka ya dini hiyo kukiwemo kujisitiri. Ni kutokana na marufuku hizo ndio maana utawala wa Aal-Saud ukatajwa kuwa utawala wa ukandamizaji na wenye kwenda sawa na hali ya karne za kati.

Tags