Algeria: Saudia ilimhonga dola milioni 2 Nabiil al Arabi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i3004-algeria_saudia_ilimhonga_dola_milioni_2_nabiil_al_arabi
Gazeti la al Shuruq la Algeria limefichua kwamba Saudi Arabia ilimhonga dola milioni mbili Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiarabu (Arab League) Nabiil al Arabi kwa akiji la kupasisha muswada wa kuitambua harakati ya Hizbullah ya Lebanon kuwa ni kundi la kigaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 13, 2016 22:54 UTC
  • Algeria: Saudia ilimhonga dola milioni 2 Nabiil al Arabi

Gazeti la al Shuruq la Algeria limefichua kwamba Saudi Arabia ilimhonga dola milioni mbili Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiarabu (Arab League) Nabiil al Arabi kwa akiji la kupasisha muswada wa kuitambua harakati ya Hizbullah ya Lebanon kuwa ni kundi la kigaidi.

Katika toleo lake la jana gazeti hilo lilifichua kuwa, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Nabiil al Arabi alipokea mlungula wa dola milioni mbili kutoka kwa serikali ya Saudia mkabala wa kupasisha muswada wa kuitambua Hizbullah kuwa ni kundi la kigaidi. Ripoti ya gazeti hilo la Algeria imenukuu duru za ndani ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuwa, katibu mkuu wa jumuiya hiyo alipewa dola milioni 9 kwa ujumla kwa anwani ya zawadi ya kumaliza muhula wake.

Azimio la hivi karibuni la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu lililoitambua harakati ya Hizbullah ya Lebanon kuwa ni kundi la kigaidi limelaani vikali na taasisi na jumuia mbalimbali kote duniani.