Uingereza: Tunaiunga mkono Saudi Arabia juu ya Qatar
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema kuwa anaiunga mkono Saudia katika mgogoro na Qatar.
Theresa May ameyasema hayo katika mazungumzo ya simu na Mohammed bin Salman al-Saud, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia ambapo sambamba na kumthibitishia uungaji mkono wa nchi yake kuhusiana na mvutano uliopo kati ya Riyadh na Doha amesema kuwa, Qatar inatakiwa ishirikiane na majirani zake wa Kiarabu kwa ajili ya kukabiliana na kile alichokitaja kuwa ni hatari ya makundi yenye misimamo mikali na ugaidi.
Kadhalika Waziri Mkuu wa Uingereza amesema kuwa, pande zote za mvutano ni lazima zifanye juhudi kwa ajili ya kupunguza mgogoro ili kuhuisha umoja wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi. Baada ya kumalizika muhula wa masharti 13 iliyopewa Qatar na nchi nne za Kiarabu, hivi sasa dunia inasubiri hatua mpya itakayochukuliwa na Saudia na waitifaki wake kuhusu nchi hiyo jirani.
Hii ni katika hali ambayo hadi sasa Waziri wa Ulinzi wa Qatar amesema kuwa, jeshi la nchi hiyo liko tayari kulilinda taifa hilo endapo itakabiliwa na chokochoko tarajiwa za maadui. Khalid al-Attiyah Waziri wa Ulinzi wa Qatar amesema nchi yake iko katika hali ya tahadhari kamili kijeshi kwa ajili ya kuhijami.