Al-Assad: Wasyria wamewashinda magaidi kwa umoja na mshikamano
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i31350-al_assad_wasyria_wamewashinda_magaidi_kwa_umoja_na_mshikamano
Rais Bashara al-Assad wa Syria amesema kuwa, Wasyria wameweza kuyashinda makundi ya kigaidi yanayowakufurisha Waislamu kwa umoja na mshikamano wao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 04, 2017 23:36 UTC
  • Al-Assad: Wasyria wamewashinda magaidi kwa umoja na mshikamano

Rais Bashara al-Assad wa Syria amesema kuwa, Wasyria wameweza kuyashinda makundi ya kigaidi yanayowakufurisha Waislamu kwa umoja na mshikamano wao.

Rais Bashar al-Assad ameyasema hayo leo alipokutana na Yousef Al-Absi, askofu wa Wakristo wa Roman Katoliki wa Antakya na maeneo Mengine wa Mashariki mwa Dunia na kusema kuwa, lengo la vita nchini Syria ni kusambaratisha misingi ya kijamii, mshikamano na umoja ambao umekuwepo kwa kipindi chote cha karne zilizopita.

Wakati magaidi wa Kiwahabi walipokuwa wakiingia Syia

Rais wa Syria ameongeza kuwa, amepongeza mchango wa kanisa katika kuimarisha umoja wa kitaifa nchini Syria katika vipindi vyote hususan katika kipindi cha vita vya sasa na kuongeza kuwa: Katika kipindi hiki cha vita kanisa hilo limekuwa na nafasi muhimu ya kulingania utaifa na kukabiliana na fikra za kuchupa mipaka na kushimakana na misingi ya utaifa, umoja wa ardhi na amani ya Syria.

Katika kikao hicho, askofu Yousef Al-Absi na ujumbe ulioongozana naye amemhakikishia Rais wa Syria kuwa nchi hiyo itapata ushindi katika vita vya sasa dhidi ya njama za magaidi na kupata tena usalama na amani.

Baada ya magaidi kufurushwa nchini Syria

Mgogoro wa Syria uliibuka mwaka 2011 baada ya nchi kama Marekani, Saudia, utawala haramu wa Israel na mataifa na washirika wao kuanzisha magenge ya kigaidi na kuyatuma nchini humo kwa lengo la kumuondoa madarakani Rais Bashar-Assad.