Mauaji ya Waislamu wa Myanmar bado yanaendelea, wakimbizi wakumbwa na maradhi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i35319-mauaji_ya_waislamu_wa_myanmar_bado_yanaendelea_wakimbizi_wakumbwa_na_maradhi
Duru za habari kutoka Bangladesh zimearifu kwamba hadi sasa jeshi la serikali ya Myanmar kwa kushirikiana na Mabudha magaidi, linaendeleza mauaji na jinai kubwa dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi wa kabila la Rohingywa wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 07, 2017 00:16 UTC
  • Mauaji ya Waislamu wa Myanmar bado yanaendelea, wakimbizi wakumbwa na maradhi

Duru za habari kutoka Bangladesh zimearifu kwamba hadi sasa jeshi la serikali ya Myanmar kwa kushirikiana na Mabudha magaidi, linaendeleza mauaji na jinai kubwa dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi wa kabila la Rohingywa wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, askari wa serikali na Mabudha wenye misimamo ya kigaidi nchini Myanmar bado wanaendeleza mauaji dhidi ya Waislamu hao wanaodhulumiwa suala ambalo limewafanya watu wa jamii hiyo ya Rohingya kuendelea kukimbilia Bangladesh kwa ajili ya kuokoa maisha yao. Aidha vyombo hivyo vya habari vimeripoti habari ya kuibuka maradhi tofauti miongoni mwa wanawake na watoto wakimbizi wa jamii hiyo katika kambi za wakimbizi na kwamba maradhi hayo yanasababishwa na lishe duni.

Jeshi la Myanmar linalofanya mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu

Viongozi wa Bangladesh wametangaza kuwa, ili kuwapa hifadhi zaidi ya wakimbizi laki nane wa Rohingya walioko nchini humo serikali ya Dhaka inajiandaa kujenga kambi kubwa zaidi kwa ajili ya shughuli hiyo. Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Bangladesh amefanya safari nchini India na kukutana na viongozi wa nchi hiyo ambapo wamezungumzia hali mbaya ya kibinaadamu inayowakabili Waislamu wa jamii ya Rohinya. Mohamed Shahidul Haque, alikutana jana Ijumaa na S.J Jaishankar, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa India mjini New Delhi ambapo alisema kuwa, hali ya Waislamu hao wanaoendelea kukimbilia nchini kwake kutokana na jinai za askari na Mabudha ni mbaya sana. Kwa upande wake Jaishankar ameahidi kuipatia serikali ya Bangladesh misaada mbalimbali yakiwemo madawa, chakula na vifaa vingine vya dharura kwa ajili ya wakimbizi hao.

Marekani na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel zinahusika katika mauaji ya Waislamu hao

Aidha amemuahidi kwamba New Delhi itafanya juhudi za kufanya mazungumzo na viongozi wa Myanmar kwa ajili ya kuhitimisha mgogoro wa Waislamu wa Rohingya. Hayo yanajiri katika hali ambayo serikali ya India pia inatuhumiwa kuhusika na ukandamizaji dhidi ya Waislamu hao ambapo hivi karibuni ilitangaza azma yake ya kuwatimua watu wa jamii hiyo ya Rohingya waliokimbilia India kwa ajili ya kuokoa maisha yao.