Macron aitaka Saudi Arabia isitishe mzingiro huko Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i38177-macron_aitaka_saudi_arabia_isitishe_mzingiro_huko_yemen
Rais wa Ufaransa amemtaka mfalme wa Saudi Arabia asitishe mzingiro wa nchi yake dhidi ya Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 27, 2017 12:10 UTC
  • Macron aitaka Saudi Arabia isitishe mzingiro huko Yemen

Rais wa Ufaransa amemtaka mfalme wa Saudi Arabia asitishe mzingiro wa nchi yake dhidi ya Yemen.

Rais Emmanuel Macron amefanya mazungumzo ya simu na Mfalme Salman wa Saudi Arabia na kumtaka kuhitimisha kikamilifu mzingiro huko Yemen na kuruhusu kuingia nchini humo misaada ya kibinadamu zikiwemo bidhaa muhimu za mahitajio. 

Uhaba wa chakula Yemen kufuatia kuzingirwa nchi hiyo pande zote
 

Rais Macron wa Ufaransa ameyasema hayo katika hali ambayo Ufaransa yenyewe ambayo imeipatia Saudia silaha za kisasa kabisa imeshiriki kwa njia isiyo ya moja kwa moja katika jinai za kivita zinazofanywa huko Yemen na muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Riyadh dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu kwa muda wa miaka mitatu sasa. Ufaransa ambayo ni nchi ya tatu muuzaji mkubwa wa silaha  duniani; ni moja ya nchi kuu zinazoiuzia silaha Saudi Arabia na nchi nyingine za Kiarabu. 

Utawala wa Aal Saud ulianzisha uvamizi wa kijeshi huko Yemen mwezi Machi mwaka 2015 kwa uungaji mkono wa Marekani na baadhi ya nchi za  Magharibi na Kiarabu kwa madai ya kutaka kumrejesha madarakani kibaraka wake Rais aliyejiuzulu wa Yemen Abdu Rabbuh Mansour Hadi.  Wayemen karibu lefu 11 wameuawa na wengine wasiopungua milioni tatu wamekuwa wakimbizi huku hujuma hizo za kijeshi zikisababisha pia hasara na maafa makubwa kwa miundo mbinu ya Yemen.