Tillerson asisitiza kuendelea kuwepo wanajeshi wa Marekani huko Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i39127-tillerson_asisitiza_kuendelea_kuwepo_wanajeshi_wa_marekani_huko_syria
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amesisitiza kuendelea kuwepo wanajeshi wa nchi hiyo huko Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 18, 2018 03:37 UTC
  • Tillerson asisitiza kuendelea kuwepo wanajeshi wa Marekani huko Syria

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amesisitiza kuendelea kuwepo wanajeshi wa nchi hiyo huko Syria.

Akihutubia jana katika Chuo Kikuu cha Stanford jimboni California, Rex Tillerson amekanusha uwezekano wowote wa kuondoka kikamilifu vikosi vya Marekani huko Syria na kueleza kuwa Marekani itaendelea kuwa na wanajeshi katika nchi hiyo ya Kiarabu. Tillerson ametilia mkazo suala la kuizidishia vikwazo serikali ya Syria na kudai kuwa vikwazo hivyo na mashinikizo vitakuwa kwa maslahi ya wananchi wa Syria. Marekani ilituma wanajeshi wake huko Syria kinyume cha sheria bila ya idhini ya serikali ya nchi hiyo kwa kisingizio cha kupambana na makundi ya kigaidi. 

Wanajeshi wa Marekani nchini Syria  
 

Washington imetuma vikosi vyake kinyume cha sheria huko Syria kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi katika hali ambayo Rais wa Marekani Donald Trump hivi karibuni alidai kuwa nchi hiyo ni chanzo kikuu cha kuibuka makundi ya kigaidi likiwemo kundi la Daesh huko Syria na Iraq. Katika sehemu nyingine ya hotuba yake ya jana, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amehimiza kuzidishiwa vikwazo Korea ya Kaskazini na kuongeza kuwa chaguo la kijeshi dhidi ya Pyongyang lipo mezani. Wakati huo huo Rex Tillerson ameshambulia siasa za kieneo za Iran na kueleza kuwa Israel ni muitifaki wa Marekani katika eneo hili.