Syria yagundua silaha za kemikali za magaidi, zimetengenezwa Ujerumani na UK
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i43698-syria_yagundua_silaha_za_kemikali_za_magaidi_zimetengenezwa_ujerumani_na_uk
Jeshi la serikali ya Syria limegundua ghala la sihala za kemikali zilizotongenezwa Ujerumani na Uingereza zilizoachwa nyuma na magaidi katika mji wa Douma.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 27, 2018 04:28 UTC
  • Syria yagundua silaha za kemikali za magaidi, zimetengenezwa Ujerumani na UK

Jeshi la serikali ya Syria limegundua ghala la sihala za kemikali zilizotongenezwa Ujerumani na Uingereza zilizoachwa nyuma na magaidi katika mji wa Douma.

Shirika la habari la Sputnik limemnukuu Naibu Mwakilishi wa Russia katika Shirika la Kuzuia Silahan za Kemikali (OPCW), Ghassan Obaid akisema kuwa jeshi la nchi hiyo limegundua silaha za kemikali zilizotengenezwa Uingereza na Ujerumani katika eneo hilo la Douma.

Obaid amewataka wakaguzi wa OPCW kutembelea eneo hilo na kueleza matumaini kwamba, watathibitisha kuwa madai yaliyotolewa na Marekani na washirika wake dhidi ya serikali ya Damascus kwamba ilitumia silaha za kemikali ni ya uongo.

Awali msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia, Maria Zakharova alikuwa amesema kuwa, kumegunduliwa mapipa yenye gesi ya klorini na mabomu ya moshi yaliyotengenezwa Uingereza na Ujerumani katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwenye udhibiti wa makundi ya kigaidi huko Ghouta Mashariki nchini Syria. 

Maria Zakharova

Timu ya wataalamu ya Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) iliyotumwa Syria tarehe 14 kuchunguza madai ya kutumiwa silaha za kemikali eneo la Douma, ilitembelea kituo cha pili mjini humo Jumatano iliyopita na kuchukua sampuli kadhaa.

Marekani, Uingereza na Ufaransa mapema mwezi huu zilishambulia maeneo kadhaa ya Syria kwa kisingizio kwamba serikali ya nchi hiyo ilitumia silaha za kemikali katika mashambulizi yake dhidi ya magaidi waliokuwa Douma huko Ghouta Mashariki. Mashambulizi hayo yalifanyika kwa msingi wa madai tu ya vyombo vya habari vya Magharibi na hayakuidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.